Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam *Mhe. Paul Makonda* amehitisha *kikao* baina yake na watendaji wa Mkoa huo wakiwemo *Wakuu wa Wilaya, Mamea, Wakurugenzi wa Manispaa, Makatibu tawala na wakuu wa Idara* ili wamueleze ni kitu gani kinachowafanya *miradi ya kimkakati* ikiwemo Machinjio ya *Vingunguti* na Ufukwe wa *Coco* imechelewa kutekelezwa licha ya *Rais Dkt. John Magufuli* kutoa fedha za miradi hiyo lakini *fedha hizo zimeishia kukaa kwenye Akaunti* pasipo utekelezaji.
*RC Makonda* amesema katika mkutano huo utakaofanyika Jumatano ya *September 25* Ukumbi wa Karimjee *mtendaji atakaebainika kusababisha uzembe huo atawajibisha* hapohapo kwa mujibu wa sheria na wengine *watazuiwa mishahara yao.*
Aidha *RC Makonda* ametoa wito kwa *Wizara ya Utumishi na TAMISEMI* kutafuta *njia bora ya kuwapata wakuu wa Idara wenye uwezo wa kuleta matokeo Chanya* tofauti na sasa ambapo *wengi wao wamepanda na kuwa wakuu wa idara kwa kigezo cha kukaa kazini Muda mrefu.*
Hayo yote yamejiri leo wakati wa hafla ya *kutoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika taaluma na Michezo.*
No comments:
Post a Comment