Serikali imeanzisha miradi ya kupunguza foleni jijini Dar es Salaam ili kupambana na sumu inayozalishwa kutokana na tatizo hilo.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 21, 2019 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene wakati akizindua kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani, Simbachawene amesema Serikali ina miradi mbalimbali ya kupunguza gesi ukaa nchini.
Ameitaja baadhi ya miradi hiyo ni wa mabasi yaendayo kasi lengo likiwa ni kupunguza foleni na idadi ya magari barabarani.
Mingine ni miradi ya ujenzi wa barabara za juu itakayosaidia kupunguza muda wa kukaa barabarani.
“Ile hali iliyoko Dar es Salaam ya kukaa muda mrefu kwenye foleni inazalisha hewa ukaa nyingi. Na hivyo kwa mtu aliyeko Dar es Salaam anakula sumu kwa kiasi kikubwa sana kuliko aliyeko Dodoma kwa sasa au kijijini,” amesema.
Amesema wanaoishi Dar es Salaam hukaa husimama katika foleni kwa saa saba bila kufika anakokwenda, kubainisha kuwa ni maisha hatari kwa binadamu kuliko ya mtu anayeishi miji isiyo na changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment