Thursday, September 19, 2019

DC, ZAINABU AITAKA HALMASHAURI YA BAGAMOYO KUONGEZA KASI YA KUKUSANYA MAPATO.

Mkuu wa Wialay ya Bagamoyo, Bi Zainabu Kawawa ameitaka Halmashauri ya Bagamoyo kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na ushuru wa Serikali ili kuongeza mapato ndani ya Halmashauri hiyo.


Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Alisema katika Halmashauri mbili zilizopo wilayani humo, Halmashauri ya Chalinze inaendelea kufanya vizuri katika kukusanya mapato huku akiinyooshea kidole Halmashauri ya Bagamoyo kwa kuzorota katika ukusanyaji wa mapato.


Alisema Taasisi zote za serikali wilayani humo kwa sasa makusanyo yao ni mazuri ikilinganishwa na awali lakini Halmashauri ya Bagamoyo imerudi nyuma katika ukusanyaji wa mapato.


Aidha, aliwataka madiwani ambao katika maeneo yao ndio kuna vyanzo vya mapato kutoa ushirikiano na watendaji kata na wenyeviti wa vitongoji ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato.


Alisema Halmashauri ya Bagamoyo bado ina vyanzo vingi vya mapato ambavyo vikitumika vizuri vitaweza kuiingizia mapato Halmashauri hiyo.


Alitoa onyo kwa watumishi wa serikali ambao hawawajibiki katika nafasi zao na kwamba atakaebainika kuwa yeye ni sababu ya kushuka kwa mapato ya Halmashauri hiyo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi ili atoe maelezo ya kutosha.


Aliongeza kwa kusema kuwa, uendeshaji wa serikali unategemea mapato hivyo kuzembea katika ukusanyaji wa mapato ni kurudisha nyumba maendeleo.

Sehemu ya madiwani wa Halmashauri ya bagamoyo wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa wilaya
katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Wakuu wa idara wa Halmashauri ya bagamoyo wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa wilaya
katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Watendaji kata wa Halmashauri ya bagamoyo wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa wilaya
katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally Issa (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi Fatuma omari Latu, wakijadili jambo kwenye kikao hicho chacha Baraza la madiwani cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2018/19 kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo. 

No comments:

Post a Comment