Na
Shushu Joel, chalinze.
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani,
wamempongeza mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete kwa Utendaji wake wa
kazi katika jimbo hilo.
Kwa
kawaida wakulima walio wengi hapa nchini hutumia muda mwingi katika shughuli ya
kilimo kwenye kipindi cha masika lakini Mbunge wa Chalinze amekuwa akilima
masika na kiangazi.
Maneno
hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya
Bagamoyo, Bi. Rukia Masenga, alipokuwa akizungumza katika sherehe za
maadhimisho ya Umoja huo ambayo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji Cha Msoga,
halmashauri ya chalinze.
"Mbunge
wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika taifa
hili kutokanana na jinsi alivyosimamia maendeleo makubwa katika jimbo lake na
sisi Umuiya ya Wanawake ndani ya wilaya hii tumeridhishwa na utekelezaji wa
ilani katika Jimbo lake "Alisema Bi Rkia.
Kwa
upande wake mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amewashukuru kina
mama hao kwa kuona kile kilichokuwa kinahitajika kwa wananchi kinatekelezeka
kwa kiwango kikubwa.
Aliongeza
kuwa chalinze imetekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kutokana na kupunguza na
kumaliza yale yaliyokuwa ni changamoto kubwa kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo
ikiwemo shida kubwa ya Maji na Afya ya kina Mama na Watoto.
Akizungumzia
ujenzi wa Vituo cha afya katika Halmashauri ya Chalinze, Mh. MBunge alisema
kazi kubwa imefanyika kujenga Zahanati kila kijiji na leo ni vijiji Vichache
ambavyo Zahanati zao hazijakamilika.
Kwa
Upande wa Vituo vya Afya hali ni nzuri sana kila Kata ispokuwa kata 3 tu,
ambazo nazo ziko mbioni kwenye Ujenzi.
Kwa
Upande wa Elimu wamejenga Vyumba zaidi ya madarasa 48, Umeme umesambazaa katika
jimbo zima la Chalinze na Miundombinu ya Barabara inakwenda vizuri na Serikali
imepanga kutumia Milioni 158.5 kwa ajili ya Barabara za Mji wa Chalinze ambazo
zitajengwa kwa kiwango cha lami na madaraja madogo.
Wakati
huo huo, Mh. Mbunge Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais
Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa
ajili ya kutatua changamoto ya Maji iliyokuwa kero kubwa sana miaka ya nyuma.
Fedha
ambazo amezieleza kuwa zinakwenda kumaliza shida ya maji sio tu kwa wana Chalinze
lakini pia kwa Maeneo ya miji ya Jirani hasa Ngerengere, na Magindu kwa upande
wa Kibaha Vijijini.
Mh.
Mbunge pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstari wa mbele katika
ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndogo ndogo za halmashauri.
Hadi
sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kata mbalimbali
lakini kubwa pia ni jinsi wanavyorudisha mikopo hivyo.
Kwa
hakika nyie ni wa kipekee, mh. Mbunge alimaliza.
No comments:
Post a Comment