MBUNGE
wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete, akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Na
Shushu Joel, Chalinze.
MBUNGE
wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amempongeza Diwani wa kata ya Bwilingu
na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) katika kata hiyo, wilayani Bagamoyo
mkoani Pwani kwa utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika kata ya
Bwilingu.
Akizungumza
na viongozi hao wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mh. Kikwete alisema
kuwa kwa utekelezaji huu wa miradi ya Maendeleo kwa wananchi ni kielelezo cha
ufanisi mzuri wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi hivyo anaamini kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi yapo maneno mengi ya kuwaambia wananchi.
Katika
Ziara hiyo Mh. Mbunge amekagua na kujionea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa
maabara ya kisasa katika kituo cha afya cha Bwilingu inayoendelea kujengwa, ujenzi
wa zahanati katika Kijiji cha mdaula na Matuli, Ujenzi wa Kituo cha Ushauri
Nasaha Majengo, ujenzi wa madarasa mawili, ofisi na vyoo Matuli na Msolwa,
ujenzi wa ofisi ya kijiji cha majengo na Miundo mbinu ya kukusanya taka katika
Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze.
Katika
Ziara hiyo Mh. Mbunge ameshauri kuombwa kwa mabadiliko ya matumizi ya fedha
zilizopelekwa katika shule ya msingi Matuli kiasi cha milioni 50
kitakachopangwa kutumiwa kujenga madarasa 2 na vyoo shuleni hapo.
Katika
kikao hicho Mh. Mbunge ameshauri kuandikwa kwa barua haraka ili fedha hizo
zijenge miundo mbinu mingine inayohitajika shuleni.
Pia
mbunge huyo amewahakikishia wananchi wa Kata ya Bwilingu kuwa serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeendelea kutekeleza mahitaji
ya wananchi kwa vitendo na kuwaondoa wasiwasi katika kufikia malengo na ndoto
zao wananchi wa Kata hiyo.
"Wananchi
wenzangu tuzidisheni maombi kwa Rais wetu Dkt Magufuli kwani Jimbo la chalinze
amekuwa akilitendea haki kutokana na kila ninachomuomba anatupatia kwa
wakati"Alisema hayo Mh.Mbunge wa Chalinze huku akiainisha huduma kama
Maji, Afya, Mahitaji ya Wazee, Miundombinu n.k.
Naye
Mwenyekiti wa CCM kata ya Bwilingu Mzee Msakamali amemwambia Mbunge kuwa chama
kitaendelea kuwa kinara wa usimamizi katika shughuli zote za miradi inayoletwa
na chama cha mapinduzi na kumuhakikishia Mh.Mbunge kuwa wamejipanga vizuri kwa
ajili ya Uchaguzi huu wa Vitongoji na Vijiji.
No comments:
Post a Comment