Pichani
ni Suriani Sosopi, akiwaonesha waandishi wa habari jeraha mmoja wa Ng'ombe 3 waliokatwa miguu kwa mapanga, PICHA NA
OMARY MNGINDO.
......................................
Na
Omary Mngindo, Bwawani
Ng'ombe
12 wanaomilikiwa na Seif Lukake mkazi wa Kijiji cha Visakazi Kata ya Ubena
Chalinze, wilayani Bagamoyo Pwani, wameshambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali
za miili yao, ikiwemo watatu kuvunjwa miguu.
Tukio
hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Sept 10 kijijini hapo, ambapo inadaiwa
kwamba mifugo hiyo iliingizwa kwenye shamba la mkazi aliyetajwa kwa jina moja
tu la Daud, mtoto wa mzee Maarufu kijijini hapo aitwaye Mzee Selemani.
Wakizungumza
na Waandishi wa habari eneo la tukio, Surian Sosopi Mwenyekiti wa Chama Cha
Wafugaji (CCWT) Kata ya Ubena, alisema kuwa alipewa taarifa ya kuwepo kwa tukio
hilo, lililofanyika mbele ya Seif ambaye ndio mwenye ng'ombe hao.
"Hili
tukio nilijulishwa jana usiku, kutokana na muda huo kutokuwa rafiki sikuweza
kuja, leo asubuhi nimefika hapa na kama nilivyowaonesha, ng'ombe wapo 12 kati
ya hao watatu wamevunjwa kabisa miguu," alisema Sosopi.
Mtendaji
wa Kijiji hicho Ramadhani Tiku alisema kuwa alipigiwa simu usiku kujulishwa
tukio hilo, akawajulisha askari Mgambo ambao walifika eneo husika ambapo
waliweka ulinzi wa kuwadhibiti ng'ombe hao mpaka asubuhi.
"Daud
ndio mwenye shamba alinijuza kuwa kuna kundi la ng'ombe limeingia shambani
kwake, niliwapigia askari wa Mgambo, walifika hapa kwa ajili ya kulinda ng'ombe
hawa ambao hawawezi hata kusimama," alisema Tiku.
Aliongeza
kuwa wakati akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya usuluhishi na kufanyika
kwa tathimi, mtuhumiwa akachukua panga na kuanza kuwakatakata ng'ombe mbele ya
mmiliki huyo aliyekuwa tayari kufanya mazungumzo na kulipa gharama husika.
Sada
Mdeka Mjumbe Kamati ya usuluhishi kati ya wafugaji na wakulima alisema kuwa,
Daud amekuwa na tabia ya ubabe, na kwamba hata panapofanyika mazungu ya kusuluhisha
migongano, yeye hufika na kuwashawishi wakulima wawafukuze wafugaji.
Akizungumzia
tukio hilo, Seif mmiliki wa ng'ombe hao aliwashukuru wafugaji wenzake
waliomsikiliza, baada ya kuwaomba wasifanye fujo kwani hali ingekuwa mbaya
zaidi.
No comments:
Post a Comment