Ikiwa
imebaki siku moja kabla ya kufanyika kwa Tamasha la 14 la jinsia, TGNP Mtandao
limemtaja Balozi Mama Getrude Mongela kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 14
linalotarajiwa kuanza September 24 hadi
27, 2019.
Haya
yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Lilian Liundi wakati
akizungumza na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam.
Akifafanua
sababu za kumpa heshima Mama Mongela kuwa Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo la
14, Liundi amesema kuna sababu nyingi za kufanya hivyo lakini kubwa ni harakati
zake alizozifanya hadi kufikia hatua za kuleta mageuzi ya jinsia hapa Nchini.
“Amesema
kuwa kipekee Tanzania itakumbukwa katika historia kwa kuweka misingi ya usawa wa kijinsia na
haki za wanawake kwani katika mkutano wa Beijing Balozi Getrude mongela
aliibuka kidedea katika mkutano huo” alisema Mkurugenzi.
Katika hatua nyingi, Mkurugenzi amebainisha
kuwa zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki
Tamasha la mwaka huu.
Tamasha hilo litakaloongozwa na kauli mbiu
inayosema 'Wanaharakati wa
Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia' limeandaliwa na TGNP Mtandao kwa
kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake na usawa wa
kijinsia na wanaharakati binafsi.
Lilian Liundi amesema washiriki wa tamasha
hilo watakuwa ni pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka ndani na nje
ya nchi,viongozi mbalimbali kutoka ngazi ya halmashauri na serikali
kuu,wanaharakati na wananchi.
"Tunatarajia tamasha
la Jinsia la Mwaka huu litakuwa la kipekee kwani kitaifa na kidunia tumeanza
kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpango kazi wa Beijing ambapo
kilele chake ni mwaka 2020”
Kwa njia moja au nyingin
maandalizi ya mkutano wa Beijing yalikuwa chachu kubwa ya kuanzishwa na
kuimarishwa kwa asasi nyingi zinazotetea haki za wanawake ",alisema.
"TGNP ni
mojawapo ya asasi iliyoleta chachu kubwa ya kuunganisha wadau mbalimbali kutoka
vikundi vya wanawake,wanazuoni na mitandao ya wanawake kupata sauti ya pamoja
katika ushiriki wa mkutano wa Beijing,hivyo TGNP inaendelea kusherehekea uwepo
wake kwa zaidi ya miaka 25 sambamba na maadhimisho ya mkutano wa Beijing",alieleza Liundi.
Alisema Tamasha hilo linatoa fursa kwa asasi
za kiraia zilizoshiriki katika mchakato wa Beijing kutakafari na kusherehekea
uwepo wa asasi hizo kwa zaidi ya miaka 25 ambapo azimio na mpango kazi Beijing
ndiyo iliyoweka misingii ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kidunia.
"Katika
kuendelea kuenzi na kuthamini mchango wa Mama Getrude Mongella,TGNP na Tapo la
Ukombozi,tumeamua kumchagua Balozi Mhe. Dr. Getrude Mongella aliyeongoza
mchakato wa Beijing na pia mchakato wa 'Kuileta Beijing Nyumbani' kuwa mgeni
rasmi wa Tamasha la Jinsia mwaka huu",alifafanua Liundi.
Hata hivyo Liundi alisema mgeni maalum kutoka
serikalini atakuwa Naibu Waziri- Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto, Mhe. Dr Faustine Ndugulile.
Alibainisha kuwa tamasha hilo litahusisha
mawasilisho,mijadala ya pamoja,maonesho na warsha,kusherekea mchango wa
mashujaa wanawake katika kufikia haki na usawa wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment