Waziri wa
Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi akizungumza kwa niaba ya waziri wa viwanda na
biashara leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini
inayoendelea kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo
Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
........................
Serikali ya Tanzania kupitia sekta binafsi ipo
tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hapa nchini.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa waziri wa viwanda
na biashara, waziri wa mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi alipokuwa akizungumza na
wafanyabiashara wa nchini Misri na watanzania wakati wa ufunguzi wa wiki ya
maonesho ya kibiashara yanayofanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro)
kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
"Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa
wawekezaji hapa nchini katika sekta ya marighafi za ujenzi, nishati ya jua,
kemikali pamoja na viwanda vya uhandisi".
Nae Rais wa chemba ya wafanyabiashara hapa nchini,
Paul Koyi amesema kuwa jukumu lao ni kufanya jambo la kibiashara lisilowezekana
kuwezekana ili biashara ziweze kufanyika bila vikwazo. Pia amesema kuwa katika
kufanya biashara kunahitaji matendo zaidi na si maneno.
Amesema hii ni fursa kwa watanzania kuungana na
kufanya biashara na wamisri kwaajili ya maendeleo ya nchi pamoja na maendeleo
yao wenyewe.
Wiki ya maonesho ya biashara ya wamisri yanaendelea
kufanyika katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam
kuanzia leo Septemba 11 hadi 14, 2019.
Mkuu wa
taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy Mbenna akizungumza katika uzinduzi wa
wiki ya biashara ya Misri na Tanzania inayoendelea kufanyika jijini Dar es
Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11
hadi 14, 2019. Amesema kuwa wafanyabiashara wachukue Fursa hiyo ambapo
wafanyabiashara wa nchini Misri wamekuja nchini kuonesha biashara zao katika
mambo ya Dawa, marighafi za ujenzi, nishati ya jua, kemikali pamoja na viwanda
vya uhandisi ni fursa wa watanzania hapa nchini kujifunza.
Rais
wa chemba ya biashara, viwanda na kilimo, Paul koyi akizungumza na
wadau wa biashara wa tanzania na wamisri katika uzinduzi wa wiki ya maonesho ya
kibiashara ya wafanyabiashara wa Misri yanayoendelea kufanyika katika hoteli ya
Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11 hadi 14 jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa akizungumza katika uzinduzi wa wiki
ya maonesho ya kibiashara ya nchi ya Misri hapa nchini yanayoendelea kufanyika
katika hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam 11 hadi 14
Septemba,2019.
Waziri wa
Mambo ya nje, Ramadhan Mwinyi, Rais wa chemba ya biashara, viwanda
na kilimo, Paul koyi, Mkuu wa taasisi ya sekta binafsi (Tpsf), Zachy
Mbenna na Balozi wa Misri Nchini Tanzania, Mohamed Abdulwafa wakikata
utepe kuzinduz wa wiki ya biashara ya wamisri hapa nchini inayoendelea
kufanyika katika hoteli ya Hyatt (Kilimanjaro) kuanzia leo Septemba 11
hadi 14 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment