Thursday, September 19, 2019

SHILINGI BILIONI 179 ZA WADAU WA MAENDELEO KUPELEKA UMEME VIJIJINI.

Image may contain: 3 people, including Subira Mgalu, people smiling, people standing
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akifurahi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari Simiyu iliyopo wilayani Bariadi, baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye shule vimejengwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
......................................


Zaidi ya shilingi bilioni 179 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo kama vile nchi za Norway, Sweden, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zinatarajiwa kutumika katika mradi wa usambazaji umeme wa ujazilizi ambapo vitongoji zaidi ya 1103 vinatarajiwa kufaidika katika mikoaTisa nchini.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Septemba 18, mwaka huu wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamanenge, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu kabla hajawasha umeme.


Mikoa itakayofaidika na mradi huo ni Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Tanga, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Singida na Tabora.


Alisema, Serikali imeleta umeme wa bei nafuu nchini ili kuleta usawa katika utoaji huduma kwa wananchi wenye vipato tofauti na kwamba wananchi wote waliopitiwa na miondombinu ya umeme watapatiwa nishati hiyo.


“Kwa upande wa Wilaya ya Maswa, matarajio yetu ni kuwa, mapema mwaka 2021 vijiji vyote vya Maswa takriban 125 vitakuwa vimeshaunganishiwa umeme, tumesema hatuchangui nyumba, nyumba zote zitawekewa umeme.” Alisemaa Mgalu.


Naye mwananchi wa Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme, aliishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wa kipato cha chini kwa kuwawekea bei ya umeme ya shilingi 27,000 ambayo hata wao wameweza kuimudu na alimhakikishia Naibu Waziri kuwa, ataitumia huduma hiyo ya umeme kujiendeleza kiuchumi.


Naibu Waziri pia aliweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Simiyu iliyopo wilayani Bariadi ambayo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limejenga baadhi ya vyumba vya madarasa na aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na watumie fursa ya umeme kujisomea haswa katika nyakati za usiku.
Image may contain: 2 people, including Subira Mgalu, people smiling
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika Kijiji cha Mwamanenge wilayani Maswa mkoa a Simiyu.
Image may contain: 3 people, including Subira Mgalu, people smiling, people standing

Mwananchi katika Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akishukuru juhudi za Serikali kupeleka umeme Kijijini hapo.
Image may contain: 1 person, crowd and outdoor

Baadhi ya Wananchi katika Kijiji cha Mwamanenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipofika Kijijini hapo kuwasha umeme.

No comments:

Post a Comment