Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi
Evarist Ndikilo ametembelea na kuweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Wande Printing
and Packaging Company Ltd kilichopo Pangani Wilayani Kibaha kitakacho tengeneza
Vifungashio vya Plastiki kwa ajili ya bidhaa za viwandani, kilimo, chakula, na
sekta ya Afya.
Kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya
Shilingi bilioni 6.6 na kitatengeneze ajira 350 kitakapo kamilika
Akiweka jiwe la Msingi leo Septemba
13, 2019, Mhandisi Evarist Ndikilo amesisitiza kuwa
ataendelea kutembelea miradi kama hiyo ya viwanda katika Mkoa wa Pwani kwa kuwa
wenye viwanda hao wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Aidha,
alisema Wanatengeneza Ajira, wanalipa Kodi na Ushuru kwa Serikali na wanasaidia
Jamii inayowazunguka na kama Serikali anao wajibu wa kusikiliza na kutatua
changamoto zinazo wakabili.
Ameitaka kampuni hiyo kupanua wigo wa
uzalishaji wa vifungashio na kuwa suluhisho la changamoto za upatikanaji wa
vifungashio nchini kwa kutengeneza vifungashio mbalimbali vitakavyotumiwa na
wajasiriamali wadogo na wa kati.
Aidha, Mhandisi Ndikilo amewataka
wawekezaji wote Mkoani Pwani kuwa na mahusiano mazuri na Wafanyakazi wao, na
kuhakikisha wanaangalia maslahi yao.
No comments:
Post a Comment