Monday, September 30, 2019

MGALU ASEMA, WANAWAKE NI JESHI KUBWA.

 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, (kulia) wakijadili jambo wakati wa maadhimisho ya Umoja wa Wanawake yaliyofanyika kiwilaya katika Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, akizungumza katika maadhimisho hayo.
................................ 

Na Shushu Joel, Chalinze.

NAIBU Waziri wa Nishati Subra Mgalu ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (UWT) kupitia mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini zaidi kwa kuwa wao ni jeshi kubwa na lenye uwezo wa hali ya juu.

Akizungumza katika maadhimisho ya Umoja wa Wanawake kiwilaya yalivyofanyika katika Jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, alisema kuwa wanawake wamekuwa ni tegemeo kwenye ufanikishaji wa mambo mbalimbali ya kijamii .

"Wanawake ni jeshi kubwa na lenye kutegemewa kwenye chama na serikali hivyo kinamama tuongeze uaminifu kwenye jamii zetu ili tuzidi kuendelea kuwa nguzo zaidi" Alisema Mgalu.

Aidha amewapongeza kinana wote waliojitokeza katika sherehe hizo na kuwataka kutembea kifua mbele kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa kwani umoja wao ndio ushindi wao.

Mgalu amewataka kinamama kukumbuka wajibu wao wa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi wa CCM ili kukIfanya chama hicho kuendelea kushika dola.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo wilaya ya Bagamoyo Rukia Masenga, amempongeza Naibu Waziri huyo kwa jinsi anavyofanya kazi za umoja wa Wanawake na hasa kuwaweka kitu kimoja wanawake wa mkoa wa Pwani.

Aidha aliongeza kuwa kinamama ni jeshi linalojitambua na hivyo amemuhakikishia naibu Waziri huyo kuwa ushindi ni lazima upatikane.

No comments:

Post a Comment