Thursday, September 19, 2019

RC. LINDI APOKEA JEZI ZA MILIONI 22 KUTOKA NMB

Hadija Hassan, Lindi.

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amepokea msaada wa jezi 900 kutoka Benk ya NMB kwa ajili ya Sare za vijana wa Halaiki zenye thamani ya Sh Milioni 22 na laki 5.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika uwanja wa Ilulu uliopo Manispaa ya Lindi Mkoani humo ambayo yaliombatana na kikao cha watumishi wa taasisi zote za serikali wakiongozwa na katibu tawalawa Mkoa huo mama Rehema madenge ikiwa ni mkakati wa maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge.

Akizungumza baada ya kupoke msaada huo, Zambi alisema jezi hizo zitatumika na vijana wa halaiki katika kilele cha Mbio za mwenge zinazotarajiwa kuhitimishwa oktoba 14/2019 Mkoani humo.

Aidha, Zambi, aliushukuru uongozi wa Bank hiyo kwa moyo walio uonyesha kwa kuchangia jezi hizo huku akieleza kuwa NMB ni wadau muhimu wa maendeleo ya wananchi na kwamba imekuwa benki ya mfano kwa utoaji huduma bora kwa Wajasiriamali, wakulima kupitia Amcos na hata kwa mtu mmoja ikiwemo kutoa gawio kwa serikali na jamii.

Awali akikabidhi msaada huo meneja wa benki hiyo kanda ya kusini, Bi Janeth Shango, alisema kutokana na kutambua kwamba sherehe hizo za mwenge ni tunu kubwa katika Nchi ndio maana Bank yao ikaona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kuchangia jezi hizo.

Hata hivyo Shango libainisha kuwa NMB katika kuleta maendeleo imejikita katika masuala ya msingi ya elimu na afya kwa kuwa wanatambua umuhimu wa elimu na afya katika jamii na kuwa suala la afya pia ni pamoja na masuala ya michezo ambayo Vijana hao wa halaiki wanayafanya

No comments:

Post a Comment