Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea ngao kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation yenye makao yake makuu mkoani Morogoro, Areef Nahdi, baada ya kukamilisha kambi ya matibabu ya moyo yaliyofadhiliwa na
shirika la Sharjah Charity Group kutoka nchi za
Falme za Kiarabu chini ya The Islamic Foundation ya hapa nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyotolewa na taasisi ya The Islamic Foundation ya
hapa nchini, ikiwa ni kumpongeza kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha
huduma za matibabu ya moyo katika taasisi hiyo wakati wa kuhitimisha kambi
maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam,
anaeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Areef Mbarak
Nahdi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa zawadi daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo kwa watoto kutoka Shirika la Sharjah Charity Group kuwapongeza kwa
jitihada wanazozifanya kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa
kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI
kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed
Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpa ngao Kiongozi kutoka shirika la
Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi kuthamini mchango unaotolewa na
shirika hilo kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa
kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa
kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed
Marzooqi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya,
viongozi mbalimbali na watoto wenye magonjwa ya moyo wanaopata matibabu katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya
matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao
kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa
waziri ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi
No comments:
Post a Comment