Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa (kushoto) akimkabidhi
Raphael Maumba boksi za karatasi na miongozo kwa ajili ya chaguzi za viongozi
ndani ya Chama Cha Mapinduzi, vilivyogharimu sh. Mil. 2.5. Picha na Omary
Mngindo.
................................
Na
Omary Mngindo, Mlandizi.
MBUNGE
wa Jimbo la Kibaha Vijini Mkoa wa Pwani Humoud Jumaa, amemkabidhi Katibu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Raphael Maumba, boksi za karatasi na miongozi
mbalimbali zinazohusiana na chaguzi.
Karatasi
na miongozo hiyo itakayotumika kwa ajili ya maandalizi ya chaguzi kuanzia ndani
ya chama hicho, ni katika kuelekea kuchagua Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji,
mchakato utakaoanzia kwenye ngazi za matawi ya chama hicho.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa Maumba ambaye ni Katibu wa chama hicho wayani hapa, Jumaaa
alisema kuwa boksi hizo za karatasi pamoja na miongozo vilivyogharimu kiasi cha
shilingi milioni 2.5, vinalenga kuwaanda wanachama hao kuelekea kwenye uchaguzi
unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu.
"Nakukabidhi
boksi za karatasi kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea kwenye chaguzi
zinazokuja, sanjali na hayo pia, pokea miongozo inayotuelekeza nini cha kufanya
wakati tunaelekea kwenye chaguzi hizo, hakikisha zinafika kwenye matawi,"
alisema Jumaa.
Aidha
Jumaa aliwataka wana-CCM kila mmoja kutumia haki yake ya ndani ya chama hicho
ikiwa ni pamoja na kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali, hivyo
wajiandae na chaguzi hizo.
Kwa
upande wake Maumba akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, alimshukuru mbunge
huyo kwa msaada huo, huku akisema kwamba umewafikia wakati mwafaka kwani katika
kipindi hiki cha kuelekea chaguzi kunahitajika vitendeakazi kama hivyo.
"Nikuahidi
Mbunge kwamba msaada huu umetufikia wakati mwafaka, na kwamba zitawafikia
walengwa katika matawi yetu, ili wanachama wajifunze mambo mbalimbali
yanayohusiana na chaguzi," alisema Maumba.
No comments:
Post a Comment