Posts

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAMOSI TAREHE 29 AGOSTI 2026

Image
 

WATUMISHI WA AFYA KAGERA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

Image
  Alodia Dominick,  Bukoba,  Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola ambao umeendelea kushambulia wananchi nchini Congo, watumishi wa afya mkoani Kagera wamepatiwa mafunzo ya utayari kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola ili ikitokea  hapa nchini wawe na uelewa mpana. Mafunzo hayo ya utayari yamefanyika Augosti 26, 2026 katika hospital ya wilaya halmashauri ya Bukoba ambapo wamefanya tukio la utayari na wataalamu wa afya  wameelezwa maswala mbalimbali ikiwemo mapokezi ya mhisiwa au mgonjwa endapo akitokea katika vituo vyao. Mafunzo ya utayari yaliyotolewa kwa wataalamu wa afya ni pamoja na jinsi ya kupokea mhisiwa wa mlipuko wa ebola na wataalamu wanapopokea mhisiwa jinsi ya kumpatia matibabu/vipimo na baada ya kutoa huduma namna ya kuvua mavazi.  Baada ya kutoa mafunzo ya utayari baadhi ya wataalamu kutoka wizara ya afya na wadau wengine wa afya wamezungumza na waandishi wa habari na kueleza maelengo ya mafunzo hayo. Afisa Muuguzi w...

MADIWANI BAGAMOYO WAAGIZA MAENEO YA SERIKALI YAPIMWE.

Image
  Baraza la madiwani Halmashauri ya mji Bagamoyo, limetoa agizo kwa mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuyapima maeneo yote ya serikali ili kuepuka migogoro ya kiumiliki baada ya serikali kuwekeza katika maeneo hayo. Akisoma Taarifa ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Diwani wa kata ya Dunda Amiry Mpwimbwi, amesema kamati imetoa mapendekezo ya ununuzi na upimaji wa maeneo ya Ardhi kwaajili ya viwanja kata ya fukayosi. Wakati wa kuchangia ripoti ya kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Madiwani walikumbusha maagizo ya muda mrefu yaliyotoleawa na baraza hilo kuhusu upimaji wa maeneo ya serikali ikiwemo viwanja vya wazi, shule za msingi na sekondari pamoja na Zahanati. Wamesema Baraza hilo limeshatoa maagizo muda mrefu ya upimaji wa maeneo yote ya serikali lakini bado utekelezaji haujafanyika hali inayopelekea kuingiza fedha za miradi kwenye maeneo ambayo hayajapimwa kisheria na baadae kuzuka migogoro ya kiumiliki. Kufuatia hali hiyo,...

RAIS DKT. SAMIA, ANGALIA MBELE; TANZANIA INAKUHITAJ

Image
  RAIS DKT. SAMIA, ANGALIA MBELE; TANZANIA INAKUHITAJ Kwako Mama yangu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Assalaam aleykum warahmatullah wabarakatuh!, Shikamoo Mama! Natumai hujambo Mama yangu, na unaendelea vema na majukumu yako mazito ya kuliongoza na kulijenga Taifa letu la Tanzania. Najua dhamana uliyonayo si ndogo, na najua kila siku mbele yako inakuja na majukumu, matarajio na wakati mwingine changamoto zinazohitaji hekima, uvumilivu na moyo wa ziada. Mama Rais Samia, waswahili wanasema, “barua ni nusu ya kuonana.” Nami nimeona nikutumie barua hii ya wazi, nikitumaini maudhui yake uyapokee kama vile unavyomuona mwanao anayeketi mbele yako na kukuambia yaliyo moyoni mwake. Siandiki kwa nia ya kukufundisha uongozi, kwa sababu najua dhamana uliyonayo na uzoefu unaokufanya uwe ulipo leo. Naandika kwa sababu mimi ni Mtanzania ninayependa kuona nchi yangu ikiendelea kusonga mbele. Mama Rais Samia, nimetafakari sana yote yaliyotokea, yanayoendelea kutokea na hata yale tunayodhani ya...

SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Shaibu Ndemanga amefungua Mafunzo ya Jeshi la Akiba yanayofanyika  Kata ya Zinga Wilayani  Bagamoyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 61. Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi kwa mshauri wa Jeshi la Akiba kwa kuhakikisha Mafunzo yanafanyika kila wakati licha ya kuwa na Changamoto mbalimbali zilizopo. Pamoja na hayo pia ametoa pongezi kwa Afisa Tarafa wa Yombo pamoja na Mtendaji kata ya Zinga kwa kukubali Mafunzo hayo kufanyika Katika Kata ya Zinga pamoja na kuwapongeza wanafunzi wote waliojitokeza katika Mafunzo hayo ya jeshi la Akiba. Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kasi ya kujengwa kwa viwanda katika Kata ya Zinga ni kubwa hivyo ni fursa kwa vijana wote ambao tayari wampata Mafunzo hayo ili kuweza kupata fursa katika viwanda hivyo. Aidha Mhe Ndemanga ameeleza kuwa  kutokana na Fursa hizo ambazo tayari nyingine zinahitaji Vijana na kusema kuwa uongozi uone namna bora ya vijana hao kupata fursa katika sehemu hizo ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa Aj...

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UHAMISHO, WAKUU WA MIKOA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 27 Agosti 2026 amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa.

ASKARI POLISI WAWILI WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI PWANI.

Image
  Askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika kivuko cha watembea kwa miguu (zebra) mailimoja Kibaha. Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Pwani, askari hao waliofariki ni Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa