Thursday, August 3, 2023

CHANGAMKIENI FURSA ZA UFUGAJI WA MAJONGOO BAHARI.

Na Nurdin Ndimbe, Morogoro.

Wananchi wameshauriwa kuchangamkia fursa zilipo katika Halmashauri ya Wilaya
Bagamoyo katika ufugaji wa majongoo Bahari ili kujiongezea kipato pamoja na
kupunguza changomoto za ajira.


Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uvuvi katika Divesheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Bw Kiboko Kiondo Godson, wakati akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Halmashauri ya Bagamoyo katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Manispaa ya Morogoro, leo tarehe 3 Agosti, 2023.


Aliwafahamisha wananchi hawo kuwa, kilimo cha majongoo bahari hufanyika
kwa kutengeneza vizimba baharini vyenye ukubwa mita za mraba kuannzia 40 na
kuendelea ambapo majongoo hufugwa na kuanza kuvunwa kuanzia miezi sita na
kuendelea.


Kilimo hiki kwa sasa kina faida kubwa sana kwani mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji, mathalani kilo moja ya majongoo yaliyokaushwa kwa bei ya soko ni
si chini Ths 180,000/-. “Tuna mahitaji makubwa sana kuliko uwezo wetu hivyo
nawasihii wananchi kuchanagamkia fursa za ufugaji wa majongoo na viumbe bahari
, na soko kubwa lipo hasa Asia hasa wenzetu kule China”. Alisistiza Bw Kiondo.


Aidha alieleza mikakati ya Halmashauri ya Bagamoyo katika kuwawezesha
wananchi kuanza ufuguaji wa majongo bahari ni pamoja na kuwaelimisha wananchi namna bora ya ufugaji wa majongoo pampja na kuwahamasiha kuunda vikundi vya ufugaji wa majongoo bahari kwani kwa sasa kuna vikundi vitatu tu
vinavyojishughulisha na ufugaji huu.


Kasi ya kuunda vikundi bado ni ndogo.
tunawashauri waanzishe fursa zipo na kubwa kwani ufugaji wa majongoo hauna
gharama kubwa unaweza kufuga wakati ukiendelea na sguhuli zingine”. Alisisitiza.


Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ni moja ya Halmashauri inayozalisha majongoo bahari kama zao la biashara na kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 zaidi ya tani 1,200 ziliuzwa nje ya Nchi hasa Uchina.


Kauli mbiu ya Maonesho wa Wakulima Nanenane 2023 ni “ Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula.





 






No comments:

Post a Comment