Monday, September 30, 2019

ACT. WAZALENDO YAWASILISHA MAOMBI YA KUJIUNGA NA KESI YA KATIBA.

Na Karama Kenyunko

CHAMA cha ACT- Wazalendo kupitia bodi yake ya dhamini, wamewasilisha maombi ya kujiunga katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mkulima Dezydelius Patrick Mgoya, ambaye anahoji kuwepo kwa kikomo cha urais nchini.

Maombi hayo yamebainishwa leo Septemba 30, 2019 na Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo, Dk Eliezer Feleshi, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na maelekezo maalumu ya namna ya usikilizwaji wa pingamizi la awali la Seriali dhidi ya kesi ji Kiongozi Dk Feleshi ndiye kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo. Wengine katika kesi hiyo ni Dk. Benhajj Masoud na Seif Kulita.

Katika maombi hayo, ACT inayowakilishwa na kampuni ya uwakili ya Law Guards Advocates wamewasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura, wakiomba maombi yao yasikilizwe haraka.

Kufuatia maombi hayo, mahakama imesimamisha usikilizwaji wa kesi ya msingi na kuamua kusikiliza kwanza maombi hayo ya ACT-Wazalendo.

Jaji Feleshi ambae anaongoza jopo la majaji watau wakiwemo Dk. Benhajj Masoud na Seif Kulita amesema, maombi hayo ya ACT- Wazalendo yatasikilizwa na jaji mmoja ambaye atalitaarifu jopo hilo kuhusu uamuzi utakaofikiwa na kesi hiyo sasa itatajwa Oktoba 25 kwa ajili ya maelekezo muhimu.

Wakili wa ACT- Wazalendo, Jebra Kambole ameeleza kuwa maombi ya wateja wake yamepangwa kusikilizwa na jaji Benhajj na kwamba yamepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza keshokutwa, Jumatano, Oktoba 2, 2019.

Katika maombi hayo pamoja na mambo mengine, chama hicho kinadai kuwa ikiwa uamuzi wa kesi hiyo utapitishwa bila wao kushirikishwa kitaathirika na kwamba kina haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkulima huyo mkazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, Patrick Dezydelius Mgoya amefungua kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya ibara ya katiba inayoweka ukomo huo wa urais.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo namba 19 ya mwaka 2019 Mgoya anahoji Ibara ya 40 (2) ya Katiba ambayo inaweka ukomo wa mihula miwili tu ya miaka mitano mitano (10) ya uongozi katika nafasi hiyo ya urais.

Hivyo anaiomba mahakama hiyo itoe tamko na tafsiri ya maana sahihi na athari za masharti ya ibara hiyo.

Pia anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana dhahiri ya masharti ya Ibara ya 42(2) ya Katiba, kwa kuhusianisha na na masharti ya Ibara za 13, 21 na 22 za Katibahiyo.

Vilevile anaiomba mahakama itoe tafsiri ya maana ya Ibara hiyo ya 40(2) kwa kuhusianisha na Ibara ya 39 ya Katiba.

Katika hati yake ya kiapo kinachounga mkono kesi hiyo, Mgoya anadai kuwa lakini Ibara ya 40(2) ya Katiba inaweka ukomo wa muda wa mtu kuchaguliwa kuwa rais, kwamba mtu hawezi kuchaguli zaidi ya mara mbili kushikilia wadhifa wa uraisi

Hivyo anadai kuwa masharti ya ibara hiyo ya 40(2) yanakiuka haki za kikatiba za Ibara za 13, 21 na 22(2) za Katiba hiyohiyo kwa kutoa mihula miwili tu ya raia kuchaguliwa kuwa rais kwa ukomo wa miaka 10 tu.

Mgoya anadai kuwa ukomo uliowekwa chini ya Ibara ya 40(2) ya Katiba yanakinzana na haki ya kikatiba ya uhuru wa kushiriki katika shughuli za umma kwa kuchagua au kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na usawa mbele ya sheria chini ya Ibara ya 21 na 13

CHANZO, MICHUZI BLOG.

VIJANA MAPINGA BAGAMOYO WATAKIWA WASIWE CHANZO CHA MPASUKA.

Kaimu Katibu Uvccm Bagamoyo ndugu Omary Ally amewasihi Vijana kuwa wavumilivu hasa Katika kipindi hiki cha Uchaguzi ili kuepusha Migongano ndani ya Chama yenye kuleta Mipasuko ambayo Miaka yote ndio imewanufaisha Vyama vya upinzani kwenye Chaguzi.


Katibu huyo ameyasema hayo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni wa heshima kwenye hafla ya kuwapongeza Vijana wa kata ya Mapinga waliohitimu Mafunzo ya Ujasiriamali Katika Kambi maalum ya Vijana wilayani humo iliyofanyika kwa siku 10.


Pamoja na hayo Ndugu Omary Aliwataka Vijana hao kutembea Kifua mbele kwakua Serikali ya awamu ya Tano imefanya Mengi Makubwa katika kuleta maendeleo nchini na yote yanaonekana hivyo kila wanapokaa basi wayaseme mafanikio hayo.


“Ndugu zangu Nchi yetu kwa Sasa inaongoza miongoni mwa nchi za kusini mwaAfrika Katika kupambana na Umasikini na jitihada hizi zinachochewa sana na Kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli hivyo tuendelee kumuombea Rais wetu Kwani Sasa Taifa letu limepiga hatua kubwa kupitia yeye ” alisema Kaimu Katibu huyo.

 
Katika Hafla hiyo Diwani wa Kata ya Mapinga ndugu Ibrahim Mbonde naye alipata Nafasi ya kueleza Utekelezaji wa ilani ya CCM Katika kipindi cha miaka minne ambapo ameishukuru serikali kwa kufanikisha Ujenzi wa Zahanati pamoja na Shule mbili za Msingi pamoja na Shule ya Sekondari Kata ya Mapinga.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA DPP KUHUSU WAHUJUMU UCHUMI.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga katika picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw.Biswalo Mganga baada ya kupiga naye picha ya pamoja na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw.Biswalo Mganga baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw.Biswalo Mganga baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Dkt. Moses Kusiluka.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga kumkabidhi taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw.Biswalo Mganga akitoa muhtasari kabla ya kukabidhi taarifa ya
utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30,2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019

PICHA NA IKULU