Eng.Patrik Kibasa Mkurugenzi Souwasa |
Joyce Joliga
Songea. Bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji
safi na salama katika shule za msingi hali ambayo inachangia watoto
kunywa maji yasiyosalama kwa afya zao hivyo kujikuta wakiugua mara kwa
mara homa za matumbo,kuharisha ,UTI .
Tatizo
la ukosefu maji safi na salama mashuleni limekuwa likiwasababishia adha
wanafunzi wengi kwani baadhi wamejikuta wakishindwa kuhudhulia masomo
kutokana na kuumwa na wengine wamejikuta wakishindwa kufanya vizuri
kwenye masomo yao.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa Juni 19 2019 kwa ushirikiano wa shirika la
afya duniani WHO, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto
UNICEF, mabilioni ya watu duniani wanaendelea kutaabika kutokana na
kukosa huduma bora za maji na masuala ya usafi.
Ripoti hiyo imeainisha takwimu mpya zikionyesha kwamba mwaka 2017
watu bilioni 3 walikosa huduma za msingi kama sabuni na mahali pa kunawa
mikono nyumbani , wakiwemo karibu robo tatu yao wanapatikana katika
nchi zenye maendeleo duni.
Kila mwaka watoto 297,000 wa chini ya umri wa miaka mitano kufariki
diunia kutokana na kuhara kunakochangiwa na ukosefu wa huduma za WASH.
Kwa upande wake Diwani kata ya
Ruhuwiko Wilbert Mahundi , anasema tatizo la maji katika shule za msingi
za kata yake ni kubwa na limechangiwa na baadhi ya shule kukatiwa maji
na zingine kutokuwa na maji ya bomba na zipo ambazo zinatumia maji ya
visima.
Anasema tayari ameziagiza kamati za shule kujadili namna ya
kuhakikisha upatikanaji wa Vifaa vya kunywea maji wanafunzi na kuwekea
maji safi na salama shuleni ili kuweza kuwanusuru watoto dhidi ya
magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu,tumbo ,taifodi na UTI
Anasema,Kamati hizo zijadili n
.kamati za shule zimetakiwa kujadili namna ya
kuhakikisha upatikanaji wa Vifaa vya kunywea maji wanafunzi na kuwekea
maji safi na salama shuleni ili kuweza kuwanusuru watoto dhidi ya
magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu,tumbo ,taifodi na UTI
amna bora na kupeleka
maazimio yao kama agenda kwenye vikao vya baraza la Kata ilizijadiliwe
na kupelekwa kwenye vikao Vya baraza la madiwani zijadiliwe na kupangiwa
bajeti kwa ajili ya utekelezaji huo
Aidha ,amewataka walimu wakuu na maafisa Elimu Msingi na
sekondari waangalie changamoto za upatikanaji wa bili za maji ili
ziingizwe kwenye capitation na kwa ajili ya kupata fedha za kulipia ili
kuweza kukwepa adha ya kukatiwa maji mara kwa mara na kuwasababishia
watoto kukosa maji safi na salama shuleni.
" Huduma ya maji safi na salama ni muhimu kwa watoto wetu
ilikuweza kuwaepusha na milipuko ya magonja ya kipindu pindu ,homa za
matumbo,UTI na hivyo tunapaswa kuwalinda na kuwasaidia wakiwa
shuleni,"Alisema Mahundi
Aidha amewataka wazazi kupitia kamati na Bodi za shule
kusimamia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na Vifaa vya
kutunzia maji na vikombe Vya kunywea maji badala ya kutumia mikono
Kwa upande wake Mwanafunzi Fatuma Ally wa shule ya Msingi
Ruhuwiko anasema kwa sasa wanafunzi hawapati maji safi kwani yamekatwa
na hakuna vikombe vya kunywea maji hivyo wanatumia mikono pia hakuna
utaratibu mzuri wa upatikanaji maji safi shuleni hapo hivyo ameuomba
uongozi wa shule kuwasaidia wanafunzi wakiwa shule kupata huduma hiyo
ilikuwaepusha na maradhi ya kuharisha na kuumwa ugonjwa wa matumbo.
Naye Ibrahim Hyella mkazi wa Ruhuwiko amepongeza jitihada
ambazo zimeanza kuchukuliwa na kamati ya shule kwa kushirikiana na
Diwani huyo kuwa zitasaidia watoto kupata maji safi na salama na hivyo
kujikinga na maradhi ya mlipuko.
Mamlaka imetumia kiasi cha Tshs 117,448,700.00 kwa ununuzi wa bomba
chache, viungio vya bomba na gharama za uchimbaji naulazaji bomba kutoka kwenye
mapato yake ya ndani ili kuwafikia wateja wengi waliokuwa hawapati huduma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafina Usafi wa Mazingira Manispaa
ya Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa,amesemawateja hao wameweza
kuunganishwakatika kipindi kifupi kwa kuwa Mamlaka ilitoa punguzo maalumu kwa
wateja ili kuweza kujiunga kwa gharama nafuu kisha kuendelea kulipia gharama za
maunganisho zilizobaki kwa makubaliano maalumu ya kulipia katika kipindi cha
miezi sita kwa kuwa huduma ilikuwa imekwisha fika katika maeneo yao.Hii ni katika
kuhakikisha wananchi wote wa Manispaa ya Songea wanapata huduma ya majisafi inayotolewa
na SOUWASA kwa kuangalia kipato halisi cha Mtanzania.
Mkurugenzi Mtendaji aliongezea kufafanua kuwa Serikaliya awamu ya tano imedhamiria
kumtua mama ndoo ya maji kichwani hivyo Mamlaka inahakikisha wakazi wa Manispaa
ya Songea wanapata huduma ya majisafi na salama uhakika.
Katika kipindi hicho cha muda mfupi, Mamlaka imeweza kuwafikia wananchi
ambao maeneo yao hayakuwahi kupata huduma ya majisafi kwa kuwaunganisha kwenye
mtandao wa majisafi nakuweza kuondokanana kero ya kutembea umbali mrefu kwenda
kutafuta maji au kutumia maji yasiyo salama ambayo yaliwasababisha magonjwa
mbalimbali yaliyotokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.
Mhandisi Patrick Kibasa amesema, wateja hao wameunganishwa kati ya Julai
naDesemba 2018. Lengo ni kutoa huduma kwaasilimia 95 ifikapo mwaka 2020na kwa
sasa huduma hiyo inatolewakwa asilimia 80 kwa kata za mjini zilizopo ndani ya
Manispaa ya Songea.
Ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unakua endelevu katika Manispaa ya
Songea Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa Mamlaka inahakikisha kuwa vyanzo vya
maji vinatunzwa. Mpaka sasa jumla ya miti 2,500 imepandwa katika bonde la mto
Luhira na takribani zaidi ya miti 5,000 inategemewa kupandwa katika vyanzo vya mlima
Matogoro katika kipindi hiki cha masika.
zikiwemo shule na taasisi mbalimbali
No comments:
Post a Comment