NA
HADIJA HASSAN- LINDI
KUTOKANA
na matumizi madogo ya viuwatilifu vya zao la korosho uliojitokeza katika Msimu
wa mwaka 2018/2019 Bodi ya korosho Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti
wa Kilimo Naliendele pamoja na TPRI imeanda mafunzo ya matumizi sahii ya
viuwatilifu hivyo katika Mikoa yote inayolima zao hilo Hapa Nchini
Hayo
yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred
alipokuwa akitoa salamu za bodi hiyo katika uzinduzi wa mafunzo ya Matumizi ya
Viuwatilifu yaliyofanyika katika kata ya Maumbika Halmashauri ya Manispaa ya
Lindi Mkoani Humo
Alisema
matumizi hayo madogo ya viuwatilifu yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa
uzalishaji wa zao hilo kutoka tani laki 313,000 za mwaka 2017/2018 hadi tani
laki 214000 kwa mwaka 2018/2019.
Alisema
mafunzo hayo hasa yanalenga makundi matatu ambayo ni wakulima wa zao la
korosho, wapuliziaji wa viuwatilifu pamoja na maafisa ugani ambao baada ya
mafunzo hayo watatakiwa kuwafundisha watu wengine katika makundi yao ambao
hawakupata fursa ya kushiriki katika mafunzo hayo.
Alfred
aliongeza kuwa Bodi ya korosho kwa kutambua uhaba wa maafisa ugani iliona njia
sahihi ya kuwafikia wakulima hao kwa wingi na haraka zaidi ni kuyakutanisha
makundi hayo na kuyapa mafuzo kwani wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka
kwa wakulima kutokujua kiwatilifu sahihi kwa ugonjwa sahihi
Nae
kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Naliendele DKT, Fortunus
Kapinga alisema katika mafunzo hayo washiriki watapata fulsa ya kujifunza njia
na namna bora ya kutumia viuwatilifu, namna ya utunzaji bora wa viuwatilifu
pamoja na jinsi ya kujilinda na viwatilifu hivyo ili usipatwe na madhara wakati
wa kuvitumia
Hata
hivyo DKT Kapinga alitumia fulsa hiyo pia kuishauri Bodi ya korosho kuendelea
na utaratibu wa kuwa na mafunzo maalumu kwa maafisa ugani kila mwaka ili
kukabiliana na magonjwa mbali mbali yanayoweza kuibuka katika misimu ya zao
hilo
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa
huo Godfrey Zambi alisema pamoja na mafunzo wanayotakiwa kupatiwa washiriki hao
pia wawafundishe jinsi ya kutunza Mazingira ikiwa pamoja na Namna ya kuteketeza
vifungashio ambavyo vilitumika kuwekea viuwatilifu huku akiwataka watumiaji wa
viwatilifu hiyo kutotumia vifungashio hivyo kwa matumizi ya nyumbani
“viuwatilifu
vingi vinavifungashio, kunamifuko ya viuwatilifu vya unga, kunachupa kubwa na
ndago, tunajiuliza baada ya kupuliza tunatupa wapi? Yapo mashamba ukizunguka
unakutata na chupa zimetupwa hovyo, unakutana na mifuko tena mbaya zaidi hii
mifuko tukimaliza kupulizia tunaiyosha alafu tunatiliamaindi tunaenda kusaga
wengine wakimaliza kupuliza chupa anaosha anaweka chuvi au sukari.
Naomba
tusaidiane baada ya kuwa tumetumia viuwatilifu vifungashio hivi tunavitupa
wapi?” alieleza Ndemanga
Hata
hivyo Ndemanga alitumia fulsa hiyo kuzitaka mamlaka zinazohusika na usambazaji
wa viuwatilifu kufanya udhibiti wa uuzwaji holela wa viuwatilifu pamoja na
maeneo yanayotumika kuuzia viuwatilifu ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza
Nae
ibrahimu Ngalondola akizungumza kwa niaba ya wakulima wengine alisema kuwa
miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika zao hilo ni bei kubwa ya
viuwatilifu jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa kwa wakilima hao kushindwa
kuandaa mashamba yao kwa wakati
No comments:
Post a Comment