Monday, June 17, 2019

NMB LINDI YATAKA WAKULIMA WA KOROSHO KUCHUKUA MIKOPO.


NA HADIJA HASSAN, LINDI

BANK ya National microfinance Bank ( NMB) Tawi la Lindi imewaaasa wakulima wa zao la Korosho Mkoani Humo kuchangamkia fulsa ya Mikopo ya Pembejeo pamoja na vifaa mbali mbali vya kilimo vinavyotolewa na Bank hiyo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa Mazao yao.

Hayo yameelezwa na Meneja wa NMB- Shaabani kasali katika mafunzo ya utumiaji ya viuwatilifu Vya zao la korosho yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani humo yaliyotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania ambayo yaliwakutanisha Wakulima wa zao hilo wapuliziaji wa viuwatilifu pamoja na maafisa ugani lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi sahii ya viuwatilifu.

Kasali alisema katika kushiriki kusaidia matumizi bora ya viwatilifu benki yao inawasaidia wakulima wa zao hilo kuwawezesha kuwapatia mikopo itakayoweza kununua pembejeo pamoja na zana mbali mbali za kilimo.

Alisema katika Msimu uliopita Bank hiyo iliweza kutoa Mikopo kwa wakulima wa zao hilo zaidi ya shilingi billion 30 kwa wakulima wa ukanda wa kusini kwa ajili ya kuwawezesha kutumia viuwatilifu ili kuhakikisha mazao hayo yanapatikana.

Aidha kasali aliongeza kuwa licha ya mikopo hiyo ya pembejeo na viuwatilifu alitaja mikopo mingine inayotolewa kwa wakulima hao ni vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrekta pamoja na mashine za upuliziaji.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo alisema kuwa ili kuweza kufikiwa na fulsa hiyo ya Mikopo ni vyema kwa wakulima hao wakajisajili katika Dafutari la kudumu la wakulima itakayomuwezesha kufahamika kwa urahisi katika taarifa zao

No comments:

Post a Comment