Rais
Donald Trump wa Marekani amekutana na kiongozi wa Korea Kaskazini katika eneo
lisilo la kijeshi la mpaka wa Korea mbili ambapo viongozi hao wawili walipeana
mikono kuonesha ishara ya matumaini ya amani.
Rais wa Marekani Donald Trump na
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, wamekubaliana kuanzisha tena
mazungumzo ya nyuklia yaliyokwama hapo awali.
Katika wiki zijazo, vikosi kazi
vitaanzishwa kutoka pande zote mbili ili kuanza ukurasa mpya wa kuendeleza
amani.
Upande wa Marekani utaongozwa na
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo.
Trump hakutoa maelezo zaidi kuhusu
yale yatakayojadiliwa lakini ameeleza wazi kwamba vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini
vitaendelea kubaki kwa muda mpaka hapo itakapofikiri vinginevyo.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini
isimamishe kabisa mpango wake wa nyuklia.
Korea Kusini na Marekani pia
wanahimiza upatikane mkataba rasmi wa amani kati ya Korea Kusini na Kaskazini.
No comments:
Post a Comment