Na
Omary Mngindo, Kibaha.
WAKAZI
Mkoa wa Pwani wametakiwa kuendeleza umoja, upendo na mshikamano, ambao hauna
ubaguzi wa dini ya aina yeyote.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo, katika futari
iliyoandaliwa na mmiliki wa shule ya KIPS iliyoko Kibaha Mailimoja mkoani hapa
Alhaj Yusufu Mginanga ambae pia ni mmiliki wa hoteli Njuweni.
Alisema
kwamba dini imeendelea kuwa kichocheo cha maendeleo ya haraka nchini, kutolana
na viongozi wake kuwahimiza waumini wake katika kuzingatia upendo, umoja na
mshikamano na kuondoa utofauti ambao zinaambatana na udini.
"Nawapongeza
viongozi wa dini mkoani Pwani, baadhi yenu hivi karibuni tumesafiri kwenda
kujionea mradi mkubwa wa umeme wa maji Mto Rufiji, unaotekelezwa na serikali
chini ya Rais Dkt. John Magufuli, nawapongeza kwa kazi zenu za kuhimiza amani,
umoja, upendo na mshikamano," alisema Mhandisi Ndikilo.
Aliongeza
kwamba mradi huo unaotaraji kuinufaisha nchi yetu katika kuhakikisha kunakuwepo
na umeme wa uhakika, amewaomba viongozi wa dini wamuombee Rais aendelee kuwa na
afya njema, pia kwa kazi kubwa ya kuuanzisha mradi huo ulioasisiwa na
watangulizi wake.
"Wakoloni
hawakuupenda mradi huu, sababu kubwa ni kwamba wamejua ungeleta maendeleo
makubwa katika nchi yetu ya Tanzania, hivyo hatua ya Rais Magufuli kuuendeleza
ni kitendo cha ujasili wa hali ya juu, tuanapaswa kuunga mkono kwa kazi
hiyo," alisema Mhandisi huyo.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alhaj Mfinanga amewataka wakazi mkoani
hapa, pasipo kujali itikadi zao za dini, rangi wala siasa katika kuhakikisha
kila mmoja anamsaidia Rais Magufuli katika utekelezaji wa ujenzi wa nchi, huku
akisisitiza elimu.
Akizungumzia
shule ya KIPS, Mfinaga alisema kwamba ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa ni shule ya awali
na msingi, ambapo tangu kipindi hicho inaendelea na utoaji wa elimu na kwamba
wanafunzi wanafanya vizuri katika mithihani yao ya kuingia kidato cha kwanza.
Baadhi
ya waumini wa dini waliohudhulia futari wamemshukuru mmiliki wa shule hiyo,
huku wakimhaidi Mkuu wa Mkoa kwamba wataendelea na utoaji wa elimu katika
nyanja mbalimbali ikiwemo kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano.
No comments:
Post a Comment