Mkazi
wa anispaa ya Lindi Juma Bakari akichangia damu katika moja ya vituo vya
kutolea damu mjini humo.
NA
HADIJA HASSAN, LINDI
Kundi
la akinamama wajawazito na watoto wachanga limetajwa kuwa ndio kundi kubwa
lenye mahitaji ya Damu salama katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Lindi
sokoine.
Hayo
yamebainishwa na mtaalamu wa Maabara wa Hospitali ya Rufa ya Lindi, Diana Ngowi katika maojiano
maalumu yaliyofanywa na BAGAMOYO KWANZA BLOG ambayo ilitaka kujua hali ya
ukusanyaji wa Damu pamoja na matumizi yake katika Hospitali hiyo.
Ngowi
alisema kwa kipindi cha miezi mitatu January-machi 2019 Hospitali hiyo ilikusanya
jumla ya Lita 372 za damu huku akitaja matumizi ya Damu kwa mwezi lita 110.
Alisema
55% ya Damu inayotumika katika hospitali hiyo ni kwa ajili ya akinamama
wajawazito 20% kwa ajili ya wagonjwa wa upasuaji, 10% watoto wachanga na
asilimia 15 makundi mengine.
Ngowi
alitaja sababu kubwa ya kundi hilo kuwa na mahitaji ya damu ni matatizo wakati
wa kujifungua ambayo hupelekea upasuaji , kutokwa na damu nyingi wakati wa
kujifungua, mahudhurio hafifu ya Kliniki, kutotumia vidonge vya kuongeza damu
vinavyotolewa katika Kliniki.
Nae
Merina Bwago Mtaalamu wa Maabara wa Manispaa ya Lindi alisema kuwa licha ya
kufanya uhamasishaji kupitia radio za kijamii zilizopo mkoani hapo pamoja na
matangazo mbali mbali lakini bado jamii kubwa ya wananchi wanaoishi katika
manispaa hiyo wamekuwa na tabia ya kuchangia damu kwa matukio mfano wakati wa
kampeni au wanapokuwa na mgonjwa aliekuwa na mahitaji ya damu.
wambo
alisema kuwa hali hiyo ya uchangiaji wa Damu inawafanya wakusanye kiasi kidogo
cha damu inayotakiwa kutumika kama dharula kulingana na mahitaji ya damu
yaliyopo katika hospital hiyo Mbwambo aliongeza kuwa watu wengi hawapendi
kuchangia damu kwa kuhofia kupimwa magonjwa mbali mbali kama vile ukimwi,
kaswende, manjano na magonjwa mengine ya zinaha
“lakini
pia kuna baadhi ya vitu wanaviogopa Damu yako mpaka ije itumike imeshafanyiwa
vipimo visivyopungua vinne , ugonjwa wa presha, kaswende, ugonjwa wa manjano
ukimwi pamoja na wingi wa damu , sasa hivi vinne kidogo ni changamoto.
Watu
wengi wanaona nikienda pale si nitagundulika nina ukimwi,si nitagundulika nina
manjano bila kujua ukichangia damu kunafaida ya kujua hivyo vitu, na kuchangia
damu hulipii hela yoyote lakini ukichangia unapimwa hivyo vipimo na ukibainika
unaugojwa unapatiwa matibabu” alisema Bwambo.
Ugo
amandusi na bakari juma ni miongoni mwa vijana wachache katika manispaa ya
lindi ambao wamejiwekea utaratibu wa kuchangia Damu kila baada ya Miezi mitatu
walisema kuwa kuchangia kwao damu kumekuwa kukiwasaidia pindi wanapokuwa na
wagonjwa katika hospitali mbali mbali hapa nchini wanapokuwa na mahitaji ya
damu hutumia kadi zao za uchangiaji na kuwawekea ndugu zao.
Ugo
alisema ameamua kuchangia Damu ili kuwasaidi watu wenyemahitaji ya huduma hiyo
huku akisema kuwa kutoa kwake damu ni sawa na sadaka kubwa kwa mwenyezimungu.
Nae
Bakari Juma alitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa Manispaa hiyo kujenga tabia
ya kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye mahitaji ya Damu ikiwa ni pamoja na kundi la akina mama wajawazito na
watoto wadogo
No comments:
Post a Comment