Na Omary Mngindo, Miono
SERIKALI imeeleza kuwa, imebaini
maeneo tisa yaliyochangia kutofikiwa kwa malengo ya mfuko wa Bima ya afya CHF,
iliyolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya tiba, kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo, amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Mji Mkuu, Kata ya Miono, Halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoani
hapa, huku moja ya changamoto hiyo akiitaja kuwa ni mfumo.
Mkuu wa wilaya ya Mafia Shaibu
Mnunduma yeye amemhakikishia Mhandisi Ndikilo kwamba, atawafikishia wakuu
wenzake maagizo yote yliyotolewa ili kuboresha huduma, huku akiwataka wananchi
kuchangamkia bima kwa ajili ya kujipatia huduma ya afya.
Mganga Mkuu mkoani Pwani Dkt. Gunini
Kamba ameiambia hadhara hiyo kwamba, faida ya bima ya afya iliyoboreshwa,
mojawapo ni mgonjwa kupata huduma ngazi za Kitongoji, Kijiji Wilaya mpaka Mkoa,
tofauti na hapo awali.
Awali taarifa ya Halmashauri ya
Chalinze ikisomwa na Mganga wa halmashauri hiyo Dkt. Rahimu Hangai, imeeleza
kwamba vijiji 83 kati ya 84, tayari vimeshanunua simu, kwa ajili ya kuandikisha
wananchi, ambao watanufaika na huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment