Chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Kilwa Msoko, wilayani Kilwa mkoa wa Lindi.
Jengo la kituo cha Afya Kilwa Msoko, wilayani Kilwa mkoa wa Lindi, Picha zote Na Hadija Hassan.
..................................
NA
HADIJA HASSAN, LINDI…
Jumla
ya kina Mama wajawazito 18 kutoka katika kata ya masoko na maeneo jirani
wamefanyiwa upasuaji mkubwa katika kituo cha afya cha kilwa masoko kilichopo
katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi baada ya kukosa Huduma hiyo kwa miaka mingi.
Hayo
yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya Dkt, Daud Selema jana
alipokuwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG ilipotembelea kituoni hapo.
Dkt.
Selema Alisema upasuaji huo ni wa miezi Saba kuanzia September 2018 mpaka April
2019.
Alisema
kuwa kituo hicho cha Afya Masoko ni miongoni mwa vituo 44 vya Afya Nchini
vilivyofanyiwa ukarabati na Serikali lengo likiwa kuzingatia majengo ya Muhimu
katika utoaji wa huduma za Mama, Baba na Mtoto.
Aliongeza
kuwa, kufuatia ukarabati huo kituo hicho cha Afya kimeshaanza kutoa huduma za
upasuaji ambao ndio lengo kuu la vituo vinavyokarabatiwa ili kuweza kutoa
huduma za dharula kwa kina Mama wajawazito wanaopata changamoto wakati wa
kujifungua.
Alisema
kabla ya kufanyiwa ukarabati huo walikuwa wanalazimika kumuhamisha Mama
Mjamzito ambae ameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kumpeleka katika
Hospital ya Wilaya ambayo ipo umbali wa kilometa 30 kutoka kituo hicho cha Afya
kilipo.
“hali
hii ilikuwa ni hatari kwa usalama wa uhai kwa Mama Mjamzito mwenyewe na hata
kwa Mtoto atakae zaliwa kwani kutokana na muongozo wetu ni lazima mama huyo awe
amefikia hatua Fulani ya uchungu na tuthibitishe kwamba kweli atashindwa
kujifungua kwa kawaida ndipo tunaweza kuamua Mama huyo afanyiwe Upasuaji ambapo
hata hivyo Huduma hiyo haikuwepo” Alifafanua Dkt, Selema.
Hata
hivyo DKT, Selema aliwataka kinamama wajawazito kuwahi kituo cha Afya mapema
pindi wanapojisikia dalili za uchungu ili watakapoanza kupata matatizo madogo
madogo wakati wa kujifungua waweze kupatiwa huduma ya upasuaji mapema ili
kumuokoa mama na mtoto atakae zaliwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Baadhi ya kina Mama waliokuja kupatiwa Huduma za Matibabu
Katika Kituo hicho cha Afya akiwemo Asha Kiambi Mkazi wa Mtaa wa Mifugo kilwa
Masoko na Kibibi Duka Mkazi wa Kilwa Masoko Walisema kuwa kutolewa kwa huduma
za upasuaji Katika Kituo hicho Cha Afya kumewasaidia kupungunza gharama za
Usafiri pindi Mama mjamzito anapotakiwa kupewa Rufaa kwenda Hospital ya Wilaya.
"Hapo
zamani Kama Mgonjwa wako atapewa Rufaa kwenda Katika Hospital ya Wilaya
tulikuwa tunalazimika kuchangia Mafuta kwa ajili ya Gari ya kumbeba Mama huyo
Mjamzito lakini kwa sasa tunaishukuru Serikali kwa kutuletea huduma za Upasuaji
Katika Kituo Chetu ambapo gharama hizo sasa tutaondokana nazo"alieleza
kiambi.
"Uwepo wa Huduma hii pia umeturahisishia
kupata muda wa ziada wa kuendelea Kufanya majukumu mengine kwa wakati Mfano
Kama utapewa Rufaa ya kwenda kwenye Hospital ya Wilaya lazima itakubidi ukae
huko mpaka mgonjwa wako atakapopata nafuu na kurudi nyumbani lakini Hapa kwa
kuwa pamekuwa Karibu na nyumbani unaweza ukamuhudumia mgonjwa na Ukafanya na
mambo Mengine kulingana na Hali ya Mgonjwa wako" aliongeza Duka
No comments:
Post a Comment