Baadhi ya wakulima wa zao la Ufuta katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakishuhudia uendeshaji wa mnada wa zao hilo.
Mrajisi
msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mkoa Huo Robert Nsunza, akizungumza wakati wa mnada huo.
.................................
NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
SERIKALI
mkoani Lindi imesema haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa kiongozi
yeyote wa Chama Cha Msingi (AMCOS) atakaehujumu Mfumo wa uuzwaji wa zao la ufuta
kwa Njia ya Mnada kwa kuchanganya zao hilo pamoja na Mchanga.
Hayo
yamesema na Mrajisi msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Mkoa Huo Robert Nsunza
June 15, 2019 katika Mnada wa zao hilo uliofanyika Ghara la Chama cha Msingi
Namangale AMCOS katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
Mkoani humo.
Nsunza
alisema ili wakulima waendelee kupata bei mzuri katika zao hilo ni muhimu kwa
watendaji katika Vyama vya Ushirika kuwa makikini katika Ufuta wanaoupokea
kutoka kwa wakulima unakuwa kwenye ubora unaotakiwa.
“Serikali
haitakuwa tayari kuona mnunuzi anakutana na Ufuta ambao utakuwa umechanganywa
na mchanga , ndio maana tunawaambia viongozi katika vyama vyao kabla ya
kuupokea Ufuta kutoka kwa mkulima na kuuingiza katika ghala ni lazima ufuta huo
waumwage chini wajilidhishe ndio waupime”
Alisema
Nsunza “Hatutakuwa tayaari kuona mtu anafanya hujuma yoyote katika hili, endapo
mnunuzi atatoa taarifa kwamba amekuta mchanga ama takataka zozote katika Ufuta
alioununua, viongozi wote wa chama husika Serikali itawawajibisha” Aliongeza
Nsunza.
Nae
Makamu Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao kinachowaunganisha
wakulima wa Wilaya za Lindi, kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani Humo Rashid
Masudi aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi wa chama hicho kuhalakisha maandalizi
ya hesabu mara baada ya kukamilika kwa minada ili wakulima waweze kulipwa fedha
zao kwa wakati.
Kwa
upande wake Tadei Mbwago Mwenyekiti wa Namangale AMCOS alisema suala la kuuweka
ufuta katika hali ya usafi ni jukumu la pande zote kuanzia kwa wakulima na
wapokeaji hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ni vyema wakulima hao
wakahakikisha ufuta wao unakuwa safi kabla ya kupeleka katika maghara kwa ajili
ya kuupima ikiwa ni pamoja na kuupeta ili kuondoa majani na takataka zingine.
Akizungumza
kwa niaba ya wakulima wengine Nuru Kambanga Mkazi wa kijiji hicho cha Namangale
alisema anaishukuru Serikali kwa mfumo waliouweka wa kuuza zao hilo kwa njia ya
mnaa kwani imewafanya wauze zao hilo kwa bei mzuri ukilinganisha na misimu
iliyopita.
Katika
Mnada huo wa Pili wa Chama kikuu cha Ushilika Lindi Mwambao jumla ya Makampuni
14 yaliomba kununua Ufuta huo ambapo Kampuni 6 kati ya hizo ndio yalifanikiwa
kununua zao hilo kwa bei ya Juu ya Tsh. 2953/= na bei ya Chini 2905 ambapo
jumla ya Tani 3220 na kilo 235 ziliuzwa
Baadhi ya wakulima wa zao la Ufuta katika kijiji cha Namangale Halmashauri ya wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakishuhudia uendeshaji wa mnada wa zao hilo.
No comments:
Post a Comment