Msemaji
Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt.
Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF
bw. Abdul Njaidi.
Dkt.
Abassi (kulia), akijadiliana jambo na Bi. Eunice Chiume, (katikati), na Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi ,mara baada ya mazungumzo yao.
............................................
MSEMAJI Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan
Abbasi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwa
kuanza vizuri kutekeleza majukumu yake katika kipindi kifupi tangu kuunganishwa
kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumamosi
Juni 15, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati alipotembelewa na
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, aliyefuatana na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi.
Kwa takriban wiki nzima, Meneja huyo
amekuwa kwenye ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya
kijamii ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya Mfuko huo
ambao ni mpya baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya
PSPF, LAPF, PPF na GEPF kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.
“Tunaposikia kuwa watu wameanza kupata
mafao yao tena kwa wakati kwakweli ni jambo la faraja kwa serikali kwa hiyo
mpeleke salamu zangu kwa watendaji wote, akiwemo mtendaji mkuu wa Mfuko,
tunafarijika sana tunapoona kwamba yale malengo ya serikali kuu kuunganisha hii
mifuko ili kutoa huduma bora yametimia.” Alisema.
Dkt, Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Habari Malezeo, pia amempongeza Meneja huyo kwa uamuzi wa
kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuelimisha umma na kueleza shughuli
za Mfuko kwani hii itasaidia wanachama kujua kinachoendelea kwenye Mfuko wao.
“Huu ni Mfuko mpya, yako maswali mengi
yanayozua tashtiti na tashwishwi ambavyo kwa pamoja vinafanya kitu kinaitwa
jakamoyo ambayo ni vile mtu anaumia moyoni kumbe anakuwa tu hana taarifa
sahihi, hili nalo niwapongeze baada ya kukamilisha zile taratibu za ndani na
kuhakikisha wale wastaafu wanapata kile kilicho chao sasa kazi kubwa ni kutoa
elimu.” Amefafanua Dkt, Abassi
Aidha Dkt. Abbasi alitoa wito kwa
wastaafu na wale wastaafu watarajiwa kutambua kuwa msingi wa pensheni ni
kumuhudumia mfanyakazi anapokosa nguvu ya kufanya kazi, ama uzeeni au kutokana
na kupata madhara mengine ambayo yatafanya akose nguvu ya kufanya kazi.
“Niwakumbushe watanzia kuwa tuweke pesa
benki zile tunazohitaji kutumia leo, kesho au katika kipindi kifupi, lakini
mafao ni kwa ajili ya kukusaidia katika maisha ya baadaye, si vema umetumikia
nchi, jamii halafu baada ya kustaafu ukaishi maisha ya mashaka.” Aliasa.
Awali Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu
kwa Umma wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume alimweleza Dkt. Abassi kuwa amepata fursa
ya kutembelea vyombo vya habari ili kujenga na kuendeleza mahusiano ikiwa ni
pamoja na kuutambulisha Mfuko huo mpya kwa wadau wa sekta ya habari.
Alisema Mfuko ulianza kutekelez
amajukumu yake Agosti 1, 2018 na ndani ya miezi 6 tangu Mfuko uanze kutekeleza
majukumu hayo umeweza kulipa malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ile ya kila
mwezi kiasi cha shilingi bilioni 880, lakini pia Mfuko unaendelea na zoezi la
kuhakiki taarifa za wanachama (wastaafu) ambapo kati ya wastaafu 120,000, elfu
10,000 bado hawajahakikiwa.
“Kwa hiyo tumeeleza kuwa Mfuko
umefungua ofisi nchi nzima bara na visiwani na kwa kila mstaafu ambaye bado
hajahakiki taarifa zake afike kwenye ofisi ya PSSSF iliyo karibu naye ili
atekeleze wajibu huo wa kisheria.” Alifafanua Bi. Chiume.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto),
akipeana mikono na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume baada ya mazungumzo
yao ofisini kwa Dkt. Abassi jijini Dar es Salaam Bi. Chiume
ambaye alikuwa katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao
ya kijamii jijini Dar es Salaam, amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo
na Dkt. Abassi.
No comments:
Post a Comment