NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
BODI
ya Kaorosho Tanzania imewataka wakulima wa zao hilo kujitokeza kwa wingi
kujisajili kwenye Dafutari la kudumu la wakulima ili kupata taarifa sahihi za
wakulima wa zao hilo kwa lengo la kujua maeneo halisi ya wakulima pamoja na
mahitaji yao.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis
Alfred alipokuwa akitoa salamu za bodi hiyo katika uzinduzi wa mafunzo ya
Matumizi ya Viuwatilifu yaliyofanyika katika kata ya Maumbika Halmashauri ya
Manispaa ya Lindi Mkoani Humo.
Alfred
alisema usajili huo utawasaidia wao kama serikali kufahamu maeneo halisi ya
wakulima kuanzia anapoishi na eneo la shamba la mkulima ikiwa ni pamoja na
kufahamu mahitaji ya pembejeo za wakulima katika eneo husika.
Alisema
bodi ya korosho imeshasambaza wataalamu wa bodi hiyo kwenye wilaya zote Nchi
mzima ambazo zinalima zao hilo ili waongeze nguvunya kwa wataalamu ambao wapo
wilayani wanaohusika na ukusanyaji wa fomu hizo za usajili lengo likiwa ni kukamilisha
usajili huo ifukapo june 20 mwaka huu wa 2019.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
Huo Godfrey Zambi alisema kuwa usajili huo licha ya kumtambua mkulima lakini
pia Mkulima huyo ataweza kupatiwa kitambulisho kitakachomuwezesha kupata mkopo
katika taasisi mbali mbali za kifedha.
Alisema
jambo la usajili kwa wakulima ni muhimu kufanyika Kwani itawasaidia Serikali
kuondokana na adha ya kuhakiki wakulima hao Mara baada ya kupeleka mazao hayo
kwenye maghara kwa ajili ya mauzo pamoja na kutambua mahitaji halisi ya
pembejeo za wakulima wa zao hilo na mahitaji Mengine Kama vile Miche na mbegu
za mikorosho.
Ndemanga
aliongeza Kuwa usajili huo pia utaisaidia Serikali kuzuia mianya ya wafanya
biashara wanaowanyonya wakulima wanaonunua zao hilo kwa njia ya choma choma
(kangomba).
Hata
hivyo Ndemanga alitumia nafasi hiyo kukanusha juu ya uvumi unaoenezwa na baadhi
ya wananchi kuhusisha usajili huo na utozwaji wa kodi kwa wakulima kuwa sio
kweli, na kubainisha kuwa lengo lengo la usajili huo ni kupata taarifa za
wakulima zilizo sahihi ili Serikali ijue namna ya kuwasaidia na kuwapa huduma
No comments:
Post a Comment