Joyce Joliga Songea.
Wazazi
wameshauliwa kuacha utoro wa kuwapeleka watoto wao Kliniki ili waweze
kupata chanjo za kuwakinga na Ulemavu au vifo vinavyotokana na maradhi
mbalimbali .
Hata hivyokwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 za Shirika la afya
duniani (WHO)zinaonyesha kuwa upatikanaji wa chajo umeongezeka ambapo watoto
85% wanachanjwa ambapo zaidi ya watoto 16 walipata chanjo muhimu tatu za
kuwakinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ambayo wakati mwingine usababisha
ulemavu.
Tayari
Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kutoa chanjo ya Matone Polio,kifua kikuu kwa
watoto weny e umri chini ya miaka mitano kwa 102% katika kipindi cha
January-Machi 2019 .
Mganga
mkuu mkoa wa Ruvuma Dkt.Jair Khanga anasema hali ya utoaji chanjo kwa watoto
chini ya miaka mitano inazidi kuhimarika ambapo kwa mwaka 2018
asilimia 93 walipata chanjo hizo na kutokana na mikakati mbalimbali
waliyojiwekea idadi ya watoto waliopata kinga imepanda na
wanatarajia kufikia 130% hadi kufikia Desemba 2019.
Anasema, Chanjo hukinga maradhi,
ulemavu na vifo vitokanavyo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwa ni
pamoja na surua, homa ya ini (hepatitisi B), dondakoo, kifaduro, nimonia,
polio, kuhara kunakosababishwa na virusi vya rota, rubela na pepopunda.
Dkt.Khanga
anasema, Watoto waliopata chanjo huwa wamekingwa dhidi ya magonjwa haya hatari,
ambayo kwa kawaida huweza kusababisha ulemavu au kifo.
Anasema
,elimu iliyotolewa kwenye kampeni maalum iliyoanzishwa ya kuwaelimisha
wazazi umuhimu wa chanjo kwa watoto imesaidia wazazi na walezi kupata
uelewa na kuwapeleka watoto kupata chanjo hali ambayo imesaidia
kuongezeka kwa idadi ya waliopata chanjo hivyo kuwanusuru na magonjwa
bali mbali ikiwemo upofu, ulemavu pamoja na vifo.
Dkt.Khanga
anaeleza kuwa elimu inaendelewa kutolewa kwa jamii huduma za mkoba pia
chanjo zinapatikana kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya , hospitalini
pia commitment ya wahudumu ni kubwa wanahakikisha kila mtoto
anafikiwa.
Aidha,
ameongeza kuwa ni asilimia ya wanawake 82.2% pekee ndio wanajifungulia
hospitalini , kwenye vituo vya afya na Zahanati na asilimia 17.8%
wanajifungulia majumbani na kwa wakunga wa jadi hivyo hakuna
chanjo wanazopata na amewashauri kujifungulia Hospitali ili watoto wao
waweze kupata chanjo hizo muhimu .
Amewashauri
wazazi na walezi wa watoto wenye umri kuanzia 0- 5 miaka kuhakikisha
wanawapeleka watoto wao kliniki na kufata maelekezo yote wanayopewa na wataalam
wa afya ili kuweza kuwa na jamii yenye afya bora na salama .
kwa
upande wake Mariam Ally Mkazi Kijiji cha Lyangweni amekiri kuwepo
kwa uzembe wa baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto wao kliniki ambapo
amesema wapo ambao wanaamini madawa ya kienyeji kuwa yanawakinga watoto
wao na wapo ambao wanapuuza tu na hawana sababu ya msingi.
“kiukweli
hata mimi sikujua kama kuna umuhimu wa watoto wetu kupelekwa Kliniki ,
kutokana na kubanwa na kazi nyingi za kilimo nimekuwa mzembe naahidi
kuanzia sasa nitampeleka mwanangu Husein kliniki ili niweze kumnusuru na
magonjwa mbalimbali,”alisema
No comments:
Post a Comment