Saturday, June 29, 2019

KILWA WAFANYA UPASUAJI WA MABUSHA BURE.

Madaktari katika kituo cha Afya Kilwa Masoko wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, wakifanya upasuaji kwa wagonjwa wa Mabusha (Ngiri maji) upasuaji huo umeanza Juni 24 na kuendelea hadi Julai 03 mwaka huu 2019.

 
Baadhi ya wakazi wa Kilwa walipata huduma ya kufanyiwa upasuaji wa mabusha (Ngiri maji) kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika kituo cha Afya Kilwa Masoko wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi,
upasuaji huo umeanza Juni 24 na kuendelea hadi Julai 03 mwaka huu 2019. Picha zote Na Hadija Hassan.
 ...................................


NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Wagonjwa 250 wenye Mabusha (ngili maji) wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa katika kituo cha Afya Cha Kilwa masoko Wilayani humo.


Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidi wa kituo hicho cha Afya Masoko Dkt, Daud selema alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG Jana ofisini kwake.


Dkt, Selema alisema kuwa upasuaji huo utafanyika kwa siku kumi mfululizo kuanzia june 24 mwaka huu mpaka julai 3 mwaka huu 2019 ambapo watu wenye matatizo hayo watafanyiwa upasuaji bure.


Aidha, Dkt, Selema aliongezakuwa,  zoezi hilo la upasuaji mabusha linafanyika kwa kushirikiana na wizara ya Afya, madaktari bingwa kutoka muhimbili pamoja na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Matibabu (NIMR).


Aidha Dkt, Selema alisema kuwa tokea zoezi hilo limeanza tayari wameshafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 70 waliofika Hospitalini hapo.


Nao baadhi ya wagonjwa ambao tayari wameshafanyiwa upasuaji huo akiwemo Bakari saidi mkazi wa masoko Mtaa wa Mnazo mmoja, Abdallah Magonga mkazi wa kijiji cha Kiwawa Kilwa na Ahamedi Saidi, kwa pamoja walisema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuendesha zoenzi hilo bure.


Nae Bakari Saidi alisema tatizo hilo la Ngili maji kwake liligundulika miaka minane iliyopita ambapo anasema kuwa kutokana na gharama za upasuaji kuwa kubwa alishindwa kwenda hospitali ili kufanyiwa upasuaji huo hivyo mpango huo umeweza kumuondolea maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Abdallah Mganga alisema kuwa changamoto aliyokuwa anakabiliana nayo kabla hajafanyiwa upasuaji huo ni kuwa na homa za mara kwa mara, maumivu maeneo ya nyonga pamoja na kukosa hamu ya tendo la ndoa Huku ahmedi Saidi akiwashauri wanaume walio na matatizo kama yake kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufanyiwa upasuaji kwani ni Bure na huduma zinazotolewa zinaridhisha.


“mimi nawashauri vijana wenzangu, wazee wote walio na matatizo kama haya waje wafanye upasuaji maana hivi vizigo havina faida bora ufuge kuku nyumbani utakula nyama au utamuuza utapata pesa sasa mizigo hii itatusaidia nini? Aalimalizia kwa kuhoji.

No comments:

Post a Comment