Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki, (katikati) akikagua kiwanda cha kinachotengeneza marumaru wilayani Mkuranga.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki amewapongeza viongozi na
wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Mkoa Pwani kwa mikakati yao ya
kuwavutia wawekezaji.
Akizungumza
kwenye kijiji cha Mwanambaya baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha “Fiber
Solution” waziri Kairuki aliwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itawashika mkono ili kufanikisha
azma yao.
Aidha
Kairuki aliutaka uongozi wa kiwanda hicho
kinachomilikiwa kwa asilimia (100) na watanzania wazawa kufungua bohari Makao
makuu ya serikali Dodoma sambamba na kusambaza mikoani.
Awali mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho cha kutengeneza nyaya za mkongo Raddy Fiber Solution Ramadhani Hassan Mlanzi alisema pamoja na uzoefu na ukomavu katika teknolojia ya mawasiliano hasa mfumo wa Fiber wanakabiliwa na changamoto zikiwemo uagizaji wa bidhaa za waya na viunganishi toka nje ya nchi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema
wamevutia wawekezaji kuwekeza katika viwanda vya kilimo, uvuvi, na mifugo ambapo
hadi kufikia June 2019 wana viwanda (71) vilivyoajiri watanzania 5424 kati ya
hivyo viwanda vikubwa 12.
Munde
alimhakikishia Waziri kairuki kuwa mkakati wao ni kufanya uwekezaji kuwa endelevu
hatimaye kufanikisha kufikia uchumi wa kati kufikia (2025)
Akiwa wilayani mkuranga Kairuki alitembelea kiwanda cha marumaru MKIU kilichozinduliwa na Raisi Magufuli April 2017.
Akiwa wilayani mkuranga Kairuki alitembelea kiwanda cha marumaru MKIU kilichozinduliwa na Raisi Magufuli April 2017.
No comments:
Post a Comment