Na
Omary Mngindo, Mkuranga.
SEKRETARIET
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, ipo katika ziara
ya kikazi kwenye Kata 25, lengo likiwa ni kujenga mahusiano zaidi na yenye
tija, ndani ya chama hicho.
Katibu
wa Sekretariet hiyo Hanzuruni Mtebwa ameiambia BAGAMOYO KWANZA BLOG kwa njia ya
simu kwamba, ziara hiyo chini ya Katibu wa chama hicho wilaya Rukia Mbasha
aliyehamia wilayani humo hivi karibuni akitokea mkoani Lindi, inalenga kujenga
mahusiano ya wana-CCM hao.
Ametanabaisha
kuwa, tayari wameshazitembelea Kata saba kati 25, ambazo ni Tengelea, Vianzi,
Vikindu, Mwandege, Mkuranga, Mtambani na Mipeko ambapo pia ziara hiyo imetumika
kumtambulisha Katibu huyo mpya.
Aidha
katika kufikia malengo hayo, Sekretariet hiyo imekabidhi REJA za wanachama kwa
Mabalozi wote wenye jukumu la balozi, ili kuhakiksha wanaweka taarifa sahihi za
wanachama wanaoishi ndani ya eneo lao la uongozi.
"Sanjali
na hayo, pia tumewahimiza kuwa na vikao ikiwemo kuanza maandalizi ya uchaguzi
ujao kuanzia serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kama unavyofahamu mwishoni
kwa mwaka huu tutaanza kuchagua Wenyeviti," alisema Mtebwa.
Sanjali
na hayo, Sekretariet hiyo imempongeza Mbunge wao Abdallah Ulega, ambaye ni
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, kwa namna anavyojitoa katika kukitumikia chama
na wananchi, ambapo ameboresha jengo la sanjali na kuweka fremu za biadhara
ikiwa ni mradi wa chama hicho.
"Katika
ziara hiyo tumepokea ushuhuda kutoka kwa viongozi, waasisi na wanachama wa CCM,
juu ya jitihada za kukisaidia Chama kwa kuchangia Ujenzi wa majengo ya Chama
ambapo Mbunge Abdallah Ulega amejitoa katika hilo," alisema Mtebwa.
Akizungumzia
usajili wa wanachama kwa mfumo wa Kielekrtonic, Katibu huyo alisema kuwa katika
uzinduzi uliofanyika kila Kata, wanachama zaidi ya 100 wamasajiliwa, huku
akigusia changamoto ya uchache wa simu ambapo kila eneo kuna simu moja tu.
Kutokana
na hali hiyo, Sektretariet imeanzisha harambee iliyokusanya kiasi cha zaidi ya
shilingi milioni tano, ikiwemo ahadi pamoja na pesa taslim zitakazotumika kwa
ununuzi wa simu ili kuboresha usajili kwa wana-CCM hao.
No comments:
Post a Comment