Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa amefuturisha ofisini kwake na kuwataka
wananchi kudumisha amani iliyopo wilayani humo ili kila mmoja afanye shughuli
zake za maendeleo kwa uhuru.
Alisema
katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kila mmoja amejifunza subira, huruma
na kusamehe na kusema kuwa hali hizo zinapaswa ziendlezwe katika miezi mingine
iliyobaki.
Katika
hutuba yake mara baada kufuturu aliwataka wananchi wa wilaya ya Bagamoyo
kujitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mita unaotarajiwa kufanyika mwaka huu
ili kila mmoja ashiriki kwa nafasi yake kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo
ndani ya wilaya hiyo.
Alisema
wale wote wenye sifa wajitokeze kugombea nafasi hizo huku wananchi wote
wanapaswa kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa kujitokeza kupiga kura.
Aidha,
alisema takwimu inaonyesha Mkoa wa pwani unaongoza kwa ujenzi wa viwanda hapa
nchini na kwamba wilaya ya Bagamoyo ni miongoni mwa wilaya zenye viwanda vingi
mkoani Pwani.
Alitumia
nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi kuendelea kuwasimamia watoto waende shule
ili hatimae wapate elimu itakayowasidia kupata ajira kwenye viwanda hivyo.
Mkuu
huyo wa wilaya amemalizia kwa kuwataka wanachi wa Bagamoyo kujiandaa kuupokea
mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuingia katika wilaya hiyo Tarehe 24 Julai.
Alisema
Bagamoyo imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka katika mapokezi ya Mwenge na kwamba
kufanya vizuri huko kunatokana na umoja, mshikamano miongoni mwa wananchi na
wataalamu kutoka idra mbalimbali za serikali na watu binafsi.
Aliwataka
wananchi kuendelea na mshikamano huo ili kwa mara nyingine wilaya ya Bagamoyo
ifanye vizuri katika miradi yake ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Mbio za
Mwenge za mwaka 2019.
Katibu
wa ccm wilaya ya Bagamoyo, Salim Mtelela wa kwanza kushoto, akiwa na mzee
maarufu mjini Bagamoyo Aliy bin Nasiri (katikati na Sheikh Ramiya Muhammad Ramiay, kulia.
Waislamu
an wanachi mbalimbali wakiwa katika mstari wa kupata futari ofisini kwa mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo alipokuwa anafuturisha katika viwanja vya ofisi yake.
Waislamu
an wanachi mbalimbali wakiwa katika mstari wa kupata futari ofisini kwa mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo alipokuwa anafuturisha katika viwanja vya ofisi yake.
No comments:
Post a Comment