Wazari wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema suala la lugha ya kufundishia na
kujifunzia ni la kisera kama iliyotamkwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014.
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo
Bungeni ambapo amesema Sera hiyo imebainisha matumizi ya lugha mbili za
Kiswahili na Kiingereza ambapo lugha ya Kiswahili inatumika kufundishia katika
ngazi ya Elimu ya Awali na Msingi, Vyuo vya Ualimu ngazi ya Cheti na Vyuo vya
Ufundi Stadi wakati lugha ya Kiingereza inatumika
katika ngazi za Elimu ya Sekondari, Vyuo vya Kati ba Vyuo Vikuu.
"Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa
lugha hiyo katika masuala ya Kitafa, Kikanda na Kimataifa kwa mawasiliano na
biashara ili kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri ktk lugha hiyo,"
amesisitiza Prof. Ndalichako.
Waziri Ndalichako amesema Kutokana na
umuhimu wa lugha ya Kiingereza serikali itaendelea kutumia lugha mbili katika
kufundishia pamoja na kuimarisha matumizi ya lugha ya kiswahili ili Watanzania
wengi zaidi kunufaika na fursa zinazojitokeza nje ya nchi.
Aidha, amesisitiza kuwa Serikali
itaangalia utaratibu wa kutumia Vyuo vilivyopo kuandaa walimu wanaofundisha
shule za English Media nakuendelea kukitangaza kiswahili ikiwa ni pamoja na
kutumika ktk mikutano ya Afrika mashariki na kufundishwa nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment