Na
Omary Mngindo, Mkuranga.
SERIKALI
imeeleza kuwa ina mpango wa kutengeneza mtambo mkubwa utakaozalisha Megawati
300 za umeme, kisha kuusafirishwa kutoka mkoani Mtwara kwenda Kinyerezi jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameyasema hayo alipozungumza na wananchi wa
Kijiji cha Njopeka, Kata ya Mjawa wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, akiwa
kijijini hapo mwishoni mwa wiki, ambapo alisema hatua hiyo inalenga kuboresha
huduma ya umeme.
Aidha
alisema kuwa serikali imefanya tathmini ya fidia kwa wananchi wa maeneo ya
Rufiji, Mkuranga na Dar es Salaam ambao wamepitiwa na bomba la gesi na nguzo za
umeme, huku akiomba radhi kuchelewa kulipwa fidia, na kwamba zoezi hilo
linataraji kuanza Julai mwaka huu.
"Malipo
yataanza mwezi Julai kwa wakazi waishio Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya hapo
zoezi litaendelea tena kuanzia mwezi wa nane mpaka wa kumi na mbili mwaka huu
kwa wakazi wa maeneo ya Mkuranga, niwaombe radhi kwa kuchelewa fidia hizo"
alisema Mgalu.
Aidha
Mgalu amewataka mafundi wa shirika la umeme Kanda ya Rufiji kuweka kambi katika
eneo la Njopeka, ili kuhakikisha wanasambaza umeme katika nyumba za wananchi
sanjali na kwenye kisima cha maji, lengo likiwa ni kuboresha upatikanaji wa
maji kwa wananchi kijijini hapo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo Alhaj Abdallah Ulega,
ameelezea shukrani zake kwa serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kazi kubwa
ya usambazaji umeme jimboni mwake.
"Nikuondoe
hofu dada yangu Mgalu, Serikali kupitia wizara yenu ya Nishati mmefanyakazi
kubwa sana ya kusambaza umeme katika vijiji jimboni kwangu, nitumie fursa hii
kuishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa namna
inavyosimamia usambazaji wa nishati hii," alisema Ulega.
Nae
Mwenyekiti wa Kijijini cha Njopeka Muharami Mketo alisema kuwa tangu kijiji
hicho kianzishwe pamoja na kupitiwa na umeme mkubwa ndio kwanza wanaonja ladha
ya umeme.
No comments:
Post a Comment