Posts

RAIS DKT. SAMIA, ANGALIA MBELE; TANZANIA INAKUHITAJ

Image
  RAIS DKT. SAMIA, ANGALIA MBELE; TANZANIA INAKUHITAJ Kwako Mama yangu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Assalaam aleykum warahmatullah wabarakatuh!, Shikamoo Mama! Natumai hujambo Mama yangu, na unaendelea vema na majukumu yako mazito ya kuliongoza na kulijenga Taifa letu la Tanzania. Najua dhamana uliyonayo si ndogo, na najua kila siku mbele yako inakuja na majukumu, matarajio na wakati mwingine changamoto zinazohitaji hekima, uvumilivu na moyo wa ziada. Mama Rais Samia, waswahili wanasema, “barua ni nusu ya kuonana.” Nami nimeona nikutumie barua hii ya wazi, nikitumaini maudhui yake uyapokee kama vile unavyomuona mwanao anayeketi mbele yako na kukuambia yaliyo moyoni mwake. Siandiki kwa nia ya kukufundisha uongozi, kwa sababu najua dhamana uliyonayo na uzoefu unaokufanya uwe ulipo leo. Naandika kwa sababu mimi ni Mtanzania ninayependa kuona nchi yangu ikiendelea kusonga mbele. Mama Rais Samia, nimetafakari sana yote yaliyotokea, yanayoendelea kutokea na hata yale tunayodhani ya...

SHAIBU NDEMANGA, AFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Shaibu Ndemanga amefungua Mafunzo ya Jeshi la Akiba yanayofanyika  Kata ya Zinga Wilayani  Bagamoyo ikiwa na jumla ya wanafunzi 61. Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi kwa mshauri wa Jeshi la Akiba kwa kuhakikisha Mafunzo yanafanyika kila wakati licha ya kuwa na Changamoto mbalimbali zilizopo. Pamoja na hayo pia ametoa pongezi kwa Afisa Tarafa wa Yombo pamoja na Mtendaji kata ya Zinga kwa kukubali Mafunzo hayo kufanyika Katika Kata ya Zinga pamoja na kuwapongeza wanafunzi wote waliojitokeza katika Mafunzo hayo ya jeshi la Akiba. Mhe Mkuu wa Wilaya amesema kasi ya kujengwa kwa viwanda katika Kata ya Zinga ni kubwa hivyo ni fursa kwa vijana wote ambao tayari wampata Mafunzo hayo ili kuweza kupata fursa katika viwanda hivyo. Aidha Mhe Ndemanga ameeleza kuwa  kutokana na Fursa hizo ambazo tayari nyingine zinahitaji Vijana na kusema kuwa uongozi uone namna bora ya vijana hao kupata fursa katika sehemu hizo ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa Aj...

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI, UHAMISHO, WAKUU WA MIKOA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 27 Agosti 2026 amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa.

ASKARI POLISI WAWILI WAFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI PWANI.

Image
  Askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika kivuko cha watembea kwa miguu (zebra) mailimoja Kibaha. Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Pwani, askari hao waliofariki ni Izdory George Michael na Rehema Juma Magawa

MWENGE WA UHURU KUWASILI KAGERA AGOSTI 30, 2026

Image
  Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Kido akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo ................... MWENGE WA UHURU KUWASILI KAGERA AGOSTI 30, 2026 Na Alodia Dominick Bukoba Miradi ya maendeleo ipatayo 54 yenye thamani ya sh bilioni 23 inatarajiwa, kuwekewa mawe ya msingi, kuzinduliwa, kukaguliwa na kufunguliwa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu mkoani Kagera. Akizungumza na waandishi wa habari leo Augosti 26, 2026 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahya Kido amesema,  mwenge wa uhuru utapokelewa wilaya ya Muleba kutokea mkoa wa Geita Agosti 30,2026 na kukimbizwa katika halmadhauri nane za mkoa huo kwa umbali wa kilomita 1,230 ambapo miradi 54 yenye thamani ya sh bilioni 23 itafikiwa na mwenge huo. Kanali Kido amesema, miradi 25 itawekewa mawe ya msingi, miradi mitano itafunguliwa, miradi 11 itazinduliwa na miradi 13 itakaguliwa na miradi hiyo inajikita katika sekta ya maji, afya, elimu, miundombinu, nishati, uwezeshaji vijana kiuchumi na mazingira wezeshi kwa uwekezaj...

SAMIA: MAULID ITUKUMBUSHE KUISHI KWA UPENDO NA AMANI

Image
  SAMIA: MAULID ITUKUMBUSHE KUISHI KWA UPENDO NA AMANI Na Rashid Mtagaluka DAR ES SALAAM:  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kutumia maadhimisho ya Maulidi kutafakari maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kujifunza misingi ya upendo, wema na amani. Ujumbe huo wa Rais Samia umetolewa leo, Agosti 25, 2026, na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyemwakilisha Rais katika Baraza la Maulidi lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam. Katika ujumbe huo, Rais Samia amesema maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad yanapaswa kuwa fursa ya kuwakumbusha waumini umuhimu wa kuishi kwa upendo, amani na kutendeana mema. Amesema kutafakari maisha ya Mtume Muhammad kutawasaidia Watanzania kuona uzuri wa mafundisho yake na kuyaweka katika maisha ya kila siku. Akizungumza kwa niaba ya Rais, Dkt. Nchemba amesema serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kujenga jamii yenye maadili, ...

RAIS, DKT. SAMIA, ARIDHIA KUJIUZULU MAKAMU WA RAIS.

Image
  RAIS, DKT. SAMIA, ARIDHIA KUJIUZULU MAKAMU WA RAIS. Kufauatia kusambaa kwa Taarifa ya kujiuzu Makamu wa Rais Dkt. Emanuel Nchimbi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameridhia ombi la kujiuzulu kwake. Katika Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi leo tarehe 25 Agosti 2026, imesema taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa. Mapema hii leo tarehe 25 Agosti 2026 zimesambaa taarifa ya kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi.