Na
Hadija Hassan, Lindi.
Jumla
ya Ng'ombe 9774 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi (Mtama) Mkoani Lindi
wanatarajia kupitishwa na Kuogeshwa katika majosho mbali mbali ya Wilaya hiyo
kwa lengo la kupatiwa chanjo dhidi ya Magonjwa yaenezwayo na kupe (Ndigana
kali).
Hayo
yameelezwa na Daktari wa mifugo wa Halmashauri hiyo Dokta Joseph Sijapenda
wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuogesha Ng'ombe katika Josho la Gereza la
kingurungundwa lililopo kata ya kitomanga Wilayani humo.
Katika
uzinduzi huo jumla ya Ng'ombe 400 kutoka kata ya kitomanga na maeneo jirani ya
wilaya hiyo walipatiwa chanjo dhidi ya Magonjwa yaenezwayo na kupe.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Sijapenda lisema kuwa Halmashauri yao imepokea jumla ya
lita 54 za dawa kwa ajili ya kuwapatia Ng'ombe 9774 waliopo katika Wilaya hiyo
ambapo lita 42 ni dawa aina ya mitraz na lita 12 aina ya palanents Huku
akifafanua kuwa lengo kubwa la Serikali kuanzisha zoezi hilo ni kuhamasisha
wafugaji kuogesha Mifugo yao ili kuwa na ufugaji wenye tija.
Hata
hivyo Sijapenda aliongeza kuwa baada ya uzinduzi huo wafungaji watalazimika
kuwapeleka Ng'ombe wao kila siku za juma mosi katika majosho yaliyo karibu nao
kwa ajili ya kuogeshwa na kupatiwa kinga hiyo.
Nae
mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na uvuvi kutoka kituo cha huduma na mifugo kanda
ya kusini jostinian lutatina alisema kuwa Magonjwa ya yaenezwayo na kupe
hususani Ndigana kali ni miongoni mwa changamoto kubwa katika maendeleo ya
sekta ya Mifugo kwa kuwa yanasababisha vifo vingi vya mifugo hapa Nchini.
"hapo
mwanzo uogeshwaji wa mifugo ulikuwa unagharamiwa na Serikali ambapo wafugaji
walikuwa wanaogeshwa bure, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti na mabadiliko ya
Sera gharama za uogeshwaji zilibaki kwa wafugaji wenyewe na matokeo yake
wafugaji wengi walikosa mwamko wa kuogesha mifugo yao" alisema.
Hata
hiyo lutatina alisema kuwa Viuwatilifu hivyo vilivyotolewa na Serikali
vitatumika kama ruzuku ambapo wafugaji watalazimika kulipa shilingi mia sita 600
kwa ng'ombe mmoja kila anapokwenda kumpatia chanjo hiyo kwa kipindi cha miezi
sita ili kiasi kitakachopatikana kiweze kununua dawa zingine.
Nae
Mwenyekiti wa wafugaji kata ya kitomanga Ntima Ngusa aliishukuru Serikali kwa
kuwapatia ruzuku hiyo ya viuwatilifu kwani itapunguza gharama ya uendeshaji
katika kuhudumia mifugo yao.
Ngusa
alisema kuwa hapo awali walikuwa wanalazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu
mbili kwa ajili ya kununua dawa ya kuogesha Ng'ombe mmoja kwa siku.
Nae
mkuu wa Wilaya ya Lindi ambae ndie aliekuwa Mgeni rasm katika uzinduzi huo
aliwataka wafugaji kujitokeza kwa wingi siku zitakazopangwa kwa ajili ya
kuwapatia chanjo mifugo yao Ili waweze kunusuru mifugo yao na magonjwa.
No comments:
Post a Comment