Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja juu ya usalama na afya kwa wahariri na waandishi wa habari Dar es salaam. |
Washiriki wa semina ya siku moja juu ya usalama na afya sehemu za kazi. |
Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam
Imeelezwa kuwa usajili wa maeneo ya kazi unaofanywa OSHA,umeongezeka
zaidi ya mara 6 toka utekelezaji wa Blue Print uanze, hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji
Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, wakati akifungua mafunzo maalaumu ya usalama na Afya kwa waandishi wa
Habari Jijini Dar es salaam.
Mwenda amesema,OSHA imetekeleza maagizo ya Mhe. Rais kwa
kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma, ikiwemo kuondoa tozo na ada mbalimbali
ambazo zilikuwa mzigo kwa wawekezaji nchini.
Kaimu Mtendaji huyo wa OSHA amesema tangu utekelezaji huo Blue
Print uanze zaidi ya maaeneo ya kazi elfu kumi na sita yamesajiliwa na OSHA mpaka kufikia Juni 2019 ukilinganisha na
maeneo 3354 yaliyosajiliwa mwaka 2015/2016.
naye kwa upande wake washiriki wa mafunzo hayo wamesema
mafunzo hayo yamewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu,
na hivyo yatawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku.
No comments:
Post a Comment