Chama cha Alliance For Democratic Change’ (ADC) kimetangaza kushuriki katika uchaguzi wa serikali wa mitaa wakisisitiza kuwa hawaoni sababu ya kutoshiriki huku kuna wagombea wao ambao wamepitishwa katika uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo amesema Chama chao kitashiriki uchaguzi huo licha ya ‘figisu figisu’ zilizojitokeza zilizosababisha baadhi ya wagombea wake kukosa kuenguliwa huku akikiri kuwa baadhi yao ‘walijichanganya’ katika mchakato wa ujazaji fomu za uteuzi.
Tunao wagombea wetu ambao wamepitishwakugombeamaeneo mbalimbali, kujitoa katika uchaguzi huu ni kuwanyima haki ya wananchi ya kuchagua viongozi wanaowataka, lakini pia kuwanyima wanachama wetu haki ya kugombea. Ndiyo maana tunagombea.
No comments:
Post a Comment