Imeelezwa kuwa matumizi ya teknolojia hasa
ICT yana tija sana katika kuyafikia maendeleo.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa siku
mbili wa Geospatial Information Road Show uliofanyika jijini Dar es salaam ambao
uliwakutanisha wataalamu wa masuala ya ardhi kutoka nchini Korea na Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho, Balozi wa
Korea Kusini nchini Tanzania Tae Ick Cho amesema Teknolojia bora katika kukuza
uchumi ndiyo silaha kubwa na pekee ya kimaendeleo na yenye kuleta
ushindani katika soko la dunia na hilo litafanikiwa kam ataifa litajikita zaidi
katika kuwekeza katika teknolojia.
Amesema bila hiyo hatutaweza kushindana na
mataifa mengine yenye teknolojia ya juu, tukumbuke msemo wa ukiona vyaelea ujue
vimeundwa , hivyo hatuwezi kuendelea bila ya kuweka mbele teknolojia,
kushirikiana na kuondoa vikwazo
Amesema kwa muda mrefu Tanzania na Korea
Kusini zimekuwa na ushirikiano wa hali ya juu hasa katika masuala ya biashara
zilizoruhusu kuvuka mipaka na hiyo yote ni kwa malengo ya kukuza uchumi baina
ya nchi hizo mbili.
Pia amesema tangu kuanzishwa kwa Geospatial
Information Road Show malengo makuu ni pamoja na kuendesha semina za
kiteknolojia katika usajili ardhi, mikutano ya biashara baina ya Serikali ya
Tanzania Makampuni wakilishi ya Korea yaliyopo nchini pamoja na kupeana taarifa
mbalimbali katika masuala ya ardhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa upimaji na ramani
kutoka Wizara ya Ardhi Hamdounny Masour amesema faida ya mkutano huo ni kwamba
Taifa litaidika na taarifa mbalimbali ambazo wataalamu hao wanazo.
Amesema kupashana habari na kubadilishana
uzoefu baina ya kampuni kutoka Korea na Tanzania ni moja katika ya hatua kubwa
ambayo itasaidia nchi hizo mbili kufikia malengo.
Masour amesema kuwa kupitia mkutano huo wataendelea
kudumisha ushirikiano huo pamoja na kupeana taarifa za kisekta katika masuala
ya upimaji wa ardhi.
“Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili umekuwa wa
kindugu na kupitia Geospatial Information Road Show na Wizara ya Ardhi
tutaendelea kupeana taarifa za kisekta ili kuweza kuyafikia maendeleo”
ameeleza.
Mkutano huo uliodumu yangu 2013 umewakutanisha wadau
kutoka Wizara ya Ardhi nchini pamoja na Wizara ya Ardhi, miundombinu na usafiri
kutoka Korea pamoja na wataalamu mbalimbali yakiwemo makampuni makubwa 12
kutoka nchini Korea.
No comments:
Post a Comment