Thursday, November 7, 2019

WAANDISHI WAJIFUNZA HABARI ZA GESI ASILIA

NA HADIJA HASSAN, Dar es salaam.

SHIRIKA la Maendeleo ya Mafuta na Gesi Tanzania (ThPDC) limetoa mafunzo ya namna ya uandishi wa habari za gesi Asilia kwa Waandishi wa habari 20 wa Mikoa ya Lindi na Mtwara Mafunzo hayo ya siku moja yalianza na ziara ya kutembelea vituo viwili Vya kupokelea gesi kutoka Madimba Mkoani Mtwara na songosongo Wilayani kilwa, kituo cha Somanga Wilayani Kilwa Mkoani Lindi na Kinyerezi Jijini Dar es salaam ambapo wanahabari walipata fursa ya kufahamu shughuli mbali mbali zinazofanywa katika vituo hivyo.

Akizungumza na Bagamoyo kwanza blog Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Gesi na Mafuta TPDC Marie Mselemu alisema kuwa lengo kubwa la mafuzo hayo kwa wanahabri ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuandika vizuri habari zinazohusu masuala ya Gesi asilia.

"Kwa kuwa tasnia ya Ges ni Tasnia mpya Shirika litaendelea kutoa mafunzo ya ujuzi na uweledi kwa Wanahabari kila tunapopata fursa ili muweze kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuielezea Sekta hii lakini pia kuelimisha Umma Kwa ukaribu na ufasaha zaidi" alisema Mselemu.

Kwa upande wake Jongo Sudy mwandishi wa habari wa kituo cha Clouds TV alisema kuwa pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yamemsaidia kufahamu namna ambavyo gesi inasafirishwa kutoka kituo cha kuchimba gesi cha Songosongo Wilayani kilwa na Madimba Mkoani Mtwara kuelekea Somanga na kwenda kinyerezi.

"Kilichonifurahisha zaidi japo sio kitu cha kawaida Wakati tuko katika kituo cha Somanga tujiandae na safari ya kuelekea Dar es salaam ni pale ambapo kituo cha jirani cha Songas kilipo anza kutoa mlipuko na gesi kuvuja ndipo wanahabari tulipo taka kufahamu na kujifunza kwa vitendo zaidi Juu kile kinachoendelea " alieleza Sofia Nyarusi mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru.

No comments:

Post a Comment