Ofisa
mradi wa Taasisi ya ukuwaji kwa usawa wa maendeleo Tanzania EQUALLY FOR GRWTH
(EFG) kupitia mpango wa sauti ya mwanamke Sokoni Suzan Sitta Kulia akimkabidhi
mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi Mohamedi Lihumbo Lidume kushoto taarifa ya
mradi wao walipofanya zihara ya Mafunzo katika Manispaa hiyo jana
PICHA
NA HADIJA HASSAN.
......................................................
Na
Hadija Hassan, Lindi.
Imeelezwa
kuwa Zaidi ya asilimia 80 ya Familia za Manispaa ya Lindi Mkoani humo
zinaendeshwa kwa kipato cha akina Mama huku akina baba wakiishia vijiwe vya
kahawa na bao.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jomary Satura alipokuwa anazungumza
na viongozi mbali mbali wa Mradi wa mwanamke sokoni (EQUALLY FOR GRWTH)
walipofanya ziara ya mafunzo katika Manispaa hiyo.
Alisema
asilimia 80% ya majukumu na malezi ya familia kwa Wanandoa wa Mkoa wa Lindi hufanywa
na kina mama huku kina baba hufanya kwa asilimia 20% pekee.
Jomari
alisema ni jambo la kawaida kwa kina baba wa ukanda huo kwenda kukaa katika
vibanda vya kahawa ama kucheza bao huku kina mama ndio wakibaki na majukumu ya
kutafuta riziki na baadae kuendesha familia za nyumba zao.
Nae
ofisa maendeleo wa Manispaa hiyo Judica Sumary amekili kuwepo kwa changamoto hiyo
huku akieleza kuwa hali ya kina mama hao kuwa ndio waendeshaji wa familia huchangia
kwa kiasi kikubwa kushindwa kurejesha kwa wakati kwa mikopo inayotolewa na
Halmashauri.
"Hali
hii inatokana na uchache wa watu katika Manispaa hii ambapo hufanya mzunguuko
wa biashara kuwa mdogo hivyo kulingana na majukumu ya kifamilia mam huyo hujikuta
kiasi kidogo alichonacho hutumia katika majukumu ya kifamilia na baadae
kushindwa kufanya marejesho ya Mkopo aliochukuwa".
Awali
akitoa taarifa ya mradi wa Sauti ya mwanamke Sokoni ofisa mradi wa (EQUALLY FOR
GROWTH) Suzan Sitta alisema kuwa Lengo kubwa la kufika katika Manspaa hiyo ni
kuwahamasisha wanawake wafanya biashara kujiunga na Umoja wa wanawake sokoni wa
kimataifa.
Alisema
lengo lingine la mpango huo ni kumkomboa mwanamke mfanya biashara kwa kumjengea
uwezo wa kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia huru katika kuendesha
biashara na shughuli za soko.
Hata
hivyo alieleza kuwa katika mpango wa mradi huo zaidi ya wanawake Wafanya
biashara 1,000 katika masoko watanufaika na mradi katika maswala ya kukuza
biashara, VICOBA, haki za wanawake , ushiriki wa wanawake katika uongozi pamoja
na kujiunga katika umoja wa wanawake sokoni.
No comments:
Post a Comment