Kamishna wa uhamiaji Taifa Dr Anna Makakala, akizungumza na waandishi wa habari, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
........................................
Na
Alodia Dominick.
Kamishna
wa uhamiaji Taifa Dr Anna Makakala amesema kwa yeyote atakayekamatwa amemficha
mhamiaji haramu atakumbwa na Kifungo cha miaka ishirini jela na kutozwa faini
ya shilingi milioni 20.
Kauli
hiyo ameitoa Novemba 13, mwaka huu wa 2019 akiwa mkoani Kagera katika ziara ya
siku tatu inayolenga kuhakikisha vitendo vya wahamiaji haramu vinakomeshwa hasa
katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nov 24 mwaka huu.
Alisema
idara hiyo itahakikisha wahamiaji haramu hawavurugi uchaguzi huo na kuwa hawana
nafasi kuingia nchini kiholela kwani tayari sheria kali zipo kwa ajiri ya
kuwabana wahamiaji ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watu watakao vunja
sheria za nchi kwa kuwaingiza watu ambao sio raia wa hapa nchini.
Dr
Makakala amesema, wananchi wafahamu kuwa, wahamiaji haramu hawana nafasi ya
kuingia na kupiga kura katika nchi ya Tanzania hivyo wananchi wanapaswa kuwa
makini nao kwa kutowakaribisha vinginevyo wafuate kanuni na sheria za kuingia
nchini.
Kwa
upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti amesema kwamba,
mwaka jana wamezindua nyumba kumi za usalama lengo likiwa ni kuhamasisha jamii
kutokaribisha wageni wanaoingia nchini kihorela.
Brigedia
Gaguti ametoa wito kwa wananchi kutowakumbatia wahamiaji haramu na badala yake
waende kutoa taarifa pale wanapobaini wageni wasio halali kwenye maeneo yake.
No comments:
Post a Comment