Wednesday, November 13, 2019

TANI 1936 ZA KOROSHO ZAUZWA LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Jumala ya tani 1936 za korosho Ghafi za chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kinachojumuisha Wakulima wa Wilaya ya Lindi (Mtama) Kilwa na Manispaa ya Lindi Mkoani humo zimeuzwa katika Mnada wa kwanza wa chama hicho kwa bei ya juu ya shiringi 2701 na bei ya chini shiringi 2541.

Mnada huo umefanyika katika kata ya Chikonji Manispaa ya Lindi ambapo makampuni 14 yalijitokeza kuomba kununua zao hilo.

Akiwahutubia wananchi pamoja na wanunuzi wa Zao hilo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi aliwataka wanunuzi kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa wakati wa kununua zao hilo ikiwa ni pamoja na kulipa fedha kwa wakati.

Zambi, alisema kulingana na utaratibu wa ununuzi wa zao hilo mfanyabiashara anatakiwa kufanya malipo ndani ya siku nne baada ya mnada hivyo ni muhimu kwa wafanya biashara kuzingatia ili wakulima waweze kulipwa fedha zao kwa wakati.

Aidha, pamoja na mambo mengine alitoa msisitizo kwa viongozi wa vyama kufanya maandalizi ya miamala ya wakulima mapema na kuiwasilisha kwenye benk ili mfanya biashara atakapo fanya malipo kwa chama kikuu ziwafikie wakulima kwa haraka.

Nae mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote unaohusiana na malipo ya Wakulima utakaosababisha upotevu wa fedha kwa wakulima.

Awali akiyataja makampuni yaliyoshinda kununua korosho hizo Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza alisema kuwa miongoni mwa makampuni yaliyoshinda ni pamoja na Alphonsa company limited kg 100,000 kwa bei ya shiringi 2701, MGM kg 400,000 kwa bei ya shiringi 27000 na kg 200,000 kwa bei ya 2690, Madag kg 51,068 kwa shiringi 2653 katika Ghara la Buco,

Alphonsa kg 100,000 kwa shiringi 2701, MGM kg 400,000 kwa shiringi 2690 na Malangi kg 1003,2846 kwa bei ya 2653 katika ghara la Mtama huku ghara la nangurukuru likianza korosho zake kwa kampuni ya Day2got kg 110 kwa bei ya Shiringi 2267 na bulaya kg 89,795 kwa bei ya Shiringi 2541.

No comments:

Post a Comment