Selemani
magali
Chuo
Kikuu cha Daresalaam kimefanya mahafali yake ya 49 dulu ya pili na tatu huku
ikiwashauri wahitimu kwenda kuyafanyia kazi yote waliyojifunza ikiwemo kuwa
wabunifu na kujitengenezea ajira kwa kufanya ujasiliamali.
Mahafili
hayo ambayo yalifayonyika katika ukumbi wa mlimani city yalishuhudia wahitimu
wa digrii za uzamili, awali, astashahada na vyeti wakitunukiwa tuzo mbalimbali.
Akizungumza
kabla ya kuwatunuku wahitimu, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuuu cha Dar es salaam Prof
William A.L Anangisye alisema kwa ujumla katika mwaka 2019 wahitimu 8,313(
wanawake 3201 au asilimia 38.5) wamefuzu na wamestahili kutunukiwa tuzo mbalimbali
za Chuo kikuu cha Dare salaam.
Alisema
kwa duru la pili kulikuwa na jumla ya wanafunzi 5, 444 (wanawake 2,194 sawa na
asilimia 40.3) kati yao, 95 (wanawaker 33 sawa na asilimia 34.7) wamefuzu na
wanastahili kutunukiwa shahada ya uzamivu; 575 (wanawake 223 sawa na 38.9%) wamefuzu
na wanastahili kutunukiwa shahada za umahili; 250 (wanawake 102 sawa na 40.8%)
wamefuzu masomo ya stashahada za uzamili; na 4,276 (wanawake 1,747 sawa 40.9%)
wamefuzu na wanastahili kutunukiwa shahada za awali.
Aidha
akitoa nasaha zake kwa wanafunzi, Anangisye aliwataka wanafunzi hao kwenda kuwa
chachu ya maendeleo, akisema wameandaliwa vizuri kupambana kuleta maendeleo
kwao wenyewe na Taifa kwa ujumla na kwamba Chuo kinawategemea kwenda kuleta
mabadiliko na kukiletea heshima katika jamii.
“Mnapoondoka
hapa na kujiunga na jamii kama sehemu ya
nguvu kazi ya muhimu, mnafahamu kwamba mnaingia katika ulimwengu unaobadilika
haraka mno. Ni muhimu nanyi mkawa wepesi mno wa kujifunza mambo mapya na
kubadilika kwa haraka ili msiachwe nyuma na wakati. Ni vyema kuzingatia msingi
huu katika kutekeleza kazi zenu za kitaaluma mtakaozokuwa mkizifanyana katika
maisha yenu ya kila siku” Alisema Anangisye
Pia
amewataka wanafunzi kuwawatu wa kutafuta fursa badala ya kusubili fursa
kuwafuata jambo ambalo si rahisi kutokea kwa ulimwengu wa sasa, lakini pia
amewashauri kuacha woga na wawe na hulka ya kujaribu mambo ambayo yanaonekana
ni magumu n ahata pale watakaposhindwa kufikia mafanikio , wasife moyo, bali
waendelee kuwa na ari ya kujaribu tena na tena mpaka mafanikio yapatikane
No comments:
Post a Comment