Na
Hadija Hassan.
SERIKALI
kupitia Shirika la maendeleo ya Gesi na Mafuta Tanzania (TPDC) linakusudia
kutekeleza mradi mkubwa wa Compressive nature Gas (CNG) wa kuongeza vituo vya
Gesi iliyoshindiliwa kwa ajili ya matumizi ya kwenye Magari.
Hayo
yameelezwa na Meneja utafiti wa mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya gesi
na mafuta Tanzania (TPDC) Aristudes Katto alipokuwa akitoa maelezo kuhusu
shughuli za Mkondo wa chini wa Gesi na usambazaji kwa wateja, kwa Waandishi wa
habari waliotembelea katika kituo cha kupokelea Gesi Kinyerezi jijini Dar es
salaam.
Katto
alisema mradi huo wa Compressive nature gas (CNG) unatarajiwa kuanza mwaka huu
wa fedha wa 2019/2020 ukiwa na lengo la kuongeza vituo vingi vya kutolea huduma
pamoja na kuchochea matumizi ya Gesi kwenye Magari.
Alifafanua
kuwa tangu nchi imeanza kutumia Gesi asilia mwaka 2004 mpaka sasa kiasi
kilichotumika ni futi za ujazo Bilioni 497 huku asilimia 82% ya gesi
inayozalishwa ikitumika katika kuzalishia umeme, 17% ikitumika viwandani na
0.02 ikitumika kwa upande wa taasisi, majumbani pamoja na kwenye magari.
Aidha
Katto pia aliongeza kuwa utekelezwaji wa Mradi huo pia utahusisha Wamiliki wa
vituo vya mafuta ambao watakuwa tayari kuunganishwa katika huduma hiyo ambavyo
vitakuwa vikitumika kama vituo vya kujaza ama kubadilisha mitungi hiyo ya Gesi.
"kwenye
Mradi huu kutakuwa na vituo mama kwa maeneo ambayo yatakuwa yamepitiwa na
miundombinu ya bomba la gesi ambavyo vitatumika kusaidia kushindilia gesi, na
baadae kusafirishwa kwenye vituo vidogo ambapo hakuna miundombinu ya mabomba ya gesi na watumiaji watafika hapo
na kubadilisha mitungi yao ya gesi" alisema Katto
"Kwa
kuanzia mradi huu utaanza Jijini Dar es salaam kwa maeneo ambayo hayajafikiwa
na miundombinu ya mabomba ya gesi ikiwemo Kigamboni, Mjini kati na pembezoni
mwa Dar chalinze na kibaha ambako pia kumeonekana kuwa na wateja wengi wenye
mahitaji wa huduma hii" aliongeza Ngowi.
Kwa
upande wake Mubarak kituya Mkazi wa Temeke Jijini Dar es salaam aliipongeza
Serikali kupitia TPDC kwa kufikiria kuanzisha mradi huo huku akieleza kwamba
wamiliki wengi wa magari walikuwa wanasita kubadilisha mifumo ya kutumia mafuta
na kutumia Gesi kwenye magari yao kwa kuhofia umbali wa kwenda kubadilishia
gesi hiyo hivyo kupitia mradi huo wanachi wengi watahamasika kutumia gesi
katika magari yao
No comments:
Post a Comment