WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na Waandishi wa habari katika zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Malipo ya Serikali kupitia M-Pesa. |
WAZIRI Jafo akifafanua jambo |
- Zaidi ya wateja milioni 14 kunufaika na matumizi ya M-Pesa katika malipo ya halmashauri na manispaa kote nchini, hayo yamebainika leo Novemba 3, 2019. Dar es Salaam.
Wateja
zaidi ya milioni 14 wa Vodacom watanufaika na huduma ya malipo kwa M-Pesa
kwenda halmashauri na manispaa mbali mbali nchini. Kampuni ya Vodacom Tanzania
kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI wamefanikisha kuimarisha mfumo wa malipo
ya kifedha
kwa
kusogeza huduma ya malipo kwa M-Pesa kwa ofisi zaidi ya 127 za serikali za
mitaa nchini. Uzinduzi wa huduma hiyo, ulifanyika ofisi za Makao Makuu ya Vodacom,
Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za mitaa
(TAMISEMI),
Mheshimiwa. Suleiman Jaffo.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mh Jaffo alisitiza umuhimu wa kutumia njia za kidigitali
kama M-pesa kufanya malipo na kukusanya mapato kwani itaboresha uwekaji wa
kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvujaji na ubadhirifu wa pesa za umma
pamoja na zkuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali ndogo.
“Malipo
kutumia njia hizi za kidigitali yanapunguza muda mwingi tuliokuwa tunatumia
kupanga foleni kufanya malipo. Sasa tuna M-Pesa naamini muda huu tukaupeleka
moja kwa moja kwenye kujenga taifa na shughuli za maendeleo. Napenda
kuwapongeza Vodacom kwa kutukumbuka na sisi huku TAMISEMI.
Ninatumaini
kwamba huduma hii itawarahisishia malipo, si tu kwa wananchi bali hata nyinyi
viongozi katika kutunza hesabu zenu,usalama wa fedha pamoja na ukusanyaji fedha
kwa ujumla,” aliongeza Jaffo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa huduma ya M-Pesa, Bwana Epimack Mbeteni alisema
kupitia M-Pesa, Vodacom inategemea kufikia taasisi nyingi za serikali na
binafsi
ili kuwezesha mfumo wa malipo kuwa rahisi,fanisi na salama zaidi. “Asilimia
kubwa ya
watanzania
wanatumia M-Pesa kufanya miamala mbali mbali kama Luku, bili za maji, faini za
barabarani, ndio maana tukaona fursa kubwa ya kurahisisha malipo kwa serikali
za mitaa kutumia M-Pesa,” aliongeza Mbeteni.
Ushirikiano
huu baina ya TAMISEMI na M-Pesa utawawezesha wateja wa mtandao wa Vodacom kufanya
zaidi ya malipo 205 ya serikali za mitaa kwa urahisi na usalama zaidi.Malipo
kama vile leseni za biashara, vibali vya ujenzi, malipo ya maegesho na nyinginezo.
“Wote
tunashuhudia jinsi M-Pesa inavoendelea kubadilisha mfumo wa malipo nchini, ni
tegemeo letu kwamba, malipo katika serikali za mitaa hizi yatakuwa rahisi na
salama zadi.
Ili
kulipa kupitia M-Pesa unapiga *150*00# anachagua lipa kwa M-Pesa, alafu malipo
kwa serikali kisha anaweka namba ya kumbukumbu ambayo utapatiwa na ofisi za
serikali za mtaa au unaweza kutumia APP ya M-Pesa kufanya malipo wakati
wowote,” alifafanua Mbeteni.
No comments:
Post a Comment