DIWANI WA TENGELEA AGAWA BAISKEL NA VIFAA VYA MICHEZO

Na Shushu Joel

DIWANI wa kata ya Tengelea, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Shabani Manda amegawa baiskeli 11 kwa makatibu tawi wa chama cha mapinduzi (CCM) kwenye kata hiyo kwa lengo la kuwasaidia ili wapate wepesi wa usafiri kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza na viongozi wa chama hicho diwani Manda alisema kuwa viongozi wa chama wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kuwafikia wanachama kutokana na kukosekana kwa usafiri wa haraka hivyo baiskeli hizi zitasaidia sana.

"Baiskeli hizi naamini zitakuwa suluhisho la viongozi wa ccm kuhangaika kuwafikia wanachama wake na hivyo kazi zao zitakuwa nyepesi"Alisema.

Aliongeza kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa sidhani kama Kuna wapinzani watakao jitokeza kugombea maana utekelezaji wa ilani ya ccm umefanyika kwa 100%.

Pia diwani huyo amegawa vifaa vya michezo vya mpira wa miguu kwa timu 20 kutoka kila kitongoji.

Aidha aliongeza kuwa vifaa hivyo ni juhudi zake za kuwapenda wananchi wake kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao.

Kwa upande wake captain wa timu ya Bungizi fc Mpame Mpame amempongeza diwani huyo kwa kugawa vifaa vya michezo kwenye vitongoji vyote ili kuinua vipaji vya vijana katika kata yake.

Naye katibu wa ccm kata Tengelea Twahili Koki amempongeza diwani huyo kwa kutoa usafiri kwa viongozi wa matawi wote 11 na hivyo kupelekea kutokomeza kabisa adha ya usafiri kwa watendaji hao wa chama cha mapinduzi.

Hivyo aliongeza kuwa vifaa hivyo vitasomeka ni mali ya ccm na si diwani tena kutokana na jinsi diwani mwenyewe alivyoamua kwa viongozi hao.

Aidha amewataka makatibu tawi wote 11 waliopata baiskeli hizo kuzitunza ili kuhakikisha zinasaidia kazi za chama kama ilivyokusudiwa kufanyika.

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU