TAASISI ya Action for change (ACHA) kwa kushirikiana
na The Right way (TRW) wamefanya uzinduzi rasmi programu endelevu ya
uelimishaji jamii na uangalizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia
kufanyika nchini Novemba 24 mwaka huu.
Programu hiyo imejenga taswira kubwa ya kuona na wapiga
kura wanapata elimu ya upigaji wa kura na uwepo wa mazingira rafiki kwa wazee
na walemavu pamoja na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru ,salama na haki
kwa vyama vyote vya kisiasa.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Action for change (ACHA) Bi Martina
Kabisama alisema wao kama taasisi za kiraia wanatekeza wajibu wa
kusimamia uchaguzi huo kwa kufuata misingi maalumu ya kisheria iliyomo kwenye
katiba ya nchi kwa kupatiwa kibali husika.
"Jamii inapaswa kujua haki zao za msingi katika kuwachagua
viongozi bora wenye sifa na uwezo wa kuongoza wananchi hivyo ni fursa pekee ya
wao kuelishwa umuhimu wa chaguzi hizi sisi kama taasisi tutajikita katika
kutoa elimu kwa wapiga kura na kusimamia zoezi la uhesabuji wa kura katika
misingi ya haki," alisema Kabisama
Kabisama alisema kuwa programu hiyo ni endelevu yenye lengo la
kuwafikia makundi mbalimbali ya wananchi waliopo mijini na vijijini ambao ndio
wapiga kura wakuu katika chaguzi zijazo hivyo kuwapa elimu ni haki yao ya
msingi.
Alisema sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa inawapa fursa
makundi mbalimbali ya taasisi za kiraia kuungana kwa pamoja na serikali kwa
kushirikiana na vyombo vingine kuweza kusimamia chaguzi , kutoa elimu na
kuhakikisha demokrasia inatawala.
Alifafanua kwa kuvitaja baadhi ya vyombo watakavyo shirikiana
navyo katika uendeshaji zoezi la uchaguzi huo kuwa ni TAKUKURU, Tume ya
uchaguzi, vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi pamoja na viongozi wa dini
kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo.
Kwa upande wake Katibu wa The Right way (TRW) Gideon Mazara
alisema kuwa mchalato wa utoaji elimu kwa jamii kupitia muungano huo
utawashirisha vyombo mbalimbali vya habari ili kuhakikisha ujumbe kusudiwa
unawafikia walengwa.
Alisema kuwa wao kama taasisi wamejipanga na kudhamilia
kutembelea mikoa yote 24 ya Tanzania ili kuweza kuliendesha zoezi la hilo la
mpiga kura ikiwemo utoaji elimu, uendeshaji sambamba na uangalizi wa uhesabuji
wa kura.
No comments:
Post a Comment