Mfumuko wa bei wa Taifa waongezeka kutoka asilimia 3.4 hadi asilimia 3.6


Na Mwandishi Wetu, MAELEZO,Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019. 
Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209 
“Ongezeko hili la mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba, 2019.” Alisema Bibi. Ruth. 
Aidha amesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo hazijumuishi chakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.7 Septemba, 2019 
Fahirisi za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na mwezi Oktoba, 2019 zimepungua kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na badiliko lilivyokuwa kati ya mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019 
Alizitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirishi kuwa ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa asilimia 2.1, petrol kwa asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa kama kompyuta kwa asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi. 
Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo ndiyo mamlaka ya kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa bei kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa bei katika nchi hizo utangazwa.

Comments

Popular posts from this blog

DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.

MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.

SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.

KIKWETE AITAKA TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA CHAKULA NA UCHUMI WA BULUU